NA MWANDISHI WETU
12th August 2013
Askari hayo waliteketeza nyumba hizo kwa amri ya Mkuu wa Wilaya ya Uvinza, Hadija Nyembo kwa madai kuwa ni hifadhi ya Kijiji cha Itebula.
Nyembo amekiri kutoa amri hiyo na amewataka wananchi hao kuondoka kabla ya Agosti 31, mwaka huu.
Wakizungumza na NIPASHE jana kijijini hapo, wakazi hao walisema tukio hilo lilitokea Novemba 23, mwaka jana majira ya saa 4 asubuhi.
Walisema wamekaa katika Kijiji hicho kwa miaka 30 na familia zao zimekulia hapo. “Tunashangaa leo tunaambiwa tuondoke kwa madai kuwa tunaishi katika hifadhi ya Kijiji?”
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kijiji cha Bweru, Patriki Ruselema, alisema katika tukio hilo la Novemba mwaka jana, vitu mbalimbali viliteketea ambavyo ni karanga gunia saba, mahindi magunia 600, Sh. milioni sita, baiskeli sita, masanduku 12 ya soda 12, simu sita zilizokuwa zinachajiwa na kuku wanne walikuwa wamelalia mayai.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma, Miriam Mbaga, alisema zoezi hilo lilisimamiwa na Mkuu wa Wilaya pamoja na watalamu wengine na kwamba malalamiko hayo yanafanyiwa kazi.
Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Uvinza, Nyembo alipaulizwa kuhusiana na tukio hilo alikiri kuteketeza nyumba hizo kwa madai kuwa zilijengwa katika hifadhi ya Kijiji cha Itebula.
“Mimi baada ya kutoa amri ya kuzichoma nyumba hizo nimepiga marufuku mwananchi yeyote kulima katika hifadhi hiyo tena kwa wale ambao bado wanaishi katika hifadhi hiyo nimetoa muda wa mwezi mmoja wakulima wote waondoke mwisho ni Agosti 31, mwaka huu,” alisema.
Mbunge wa Kigoma Kusini (NCCR-Mageuzi), David Kafulila, alisema amashangazwa na DC kuwaambia polisi wachome nyumba 68 za wakulima na kwamba alipeleka malalamiko kwa Mkuu wa Mkoa lakini hakuna hatua iliyochukuliwa.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma, Frasser Kashai, alisema hajawahi kuwatuma polisi kwenda kuchoma nyumba hizo na kwamba atachunguza ili kujua kama polisi walihusika na tukio hil
CHANZO: NIPASHE
No comments :
Post a Comment