NA MWANDISHI WETU
14th August 2013
Alikuwa akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano wa 11 wa Chama cha Majaji na Mahakimu cha Afrika Mashariki (EAMJA) unaofanyika Zanzibar. Dk. Shein alisema kumekuwapo na mjadala wa muda mrefu juu ya uhusiano wa ongezeko la vitendo hivyo na ufanisi wa utendaji kazi katika vyombo vinavyosimamia utekelezaji wa sheria.
Aliongeza kuwa tatizo hilo linatajwa kuwa miongoni mwa sababu zinazokwamisha maendeleo barani Afrika.
Dk. Shein aliwataka wanachama wa EAMJA kuendelea kufanya kazi kwa karibu na vyombo vinavyosimamia utekelezaji wa sheria pamoja na jamii ili kuhakikisha sheria zinatekelezwa ili haki itendeke.
Alivitaja baadhi ya vitendo vya kihalifu ambavyo vitachukua nafasi katika mijadala ya mkutano huo kuwa ni rushwa na unyanyasaji watoto.
Hata hivyo, Dk. Shein alisema Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imejizatiti kupambana na tatizo la rushwa na imeunda mamlaka maalum ya kushughulikia suala hilo na uhalifu wa kiuchumi.
Katika mkutano huo, miongoni mwa masuala yatakayojadiliwa na kutarajiwa kuzua mjadala mkubwa ni pamoja na hukumu ya kifo na suala la utoaji mimba.
Masuala hayo yamekuwa yakichukua nafasi kubwa katika mijadala mbalimbali ya kisheria kutokana na kuwapo mitazamo tofauti na hoja mbalimbali zinazokataa au kuunga mkono zote zikihusisha haki za binadamu.
CHANZO: NIPASHE
No comments :
Post a Comment