NA MWANDISHI WETU
9th August 2013
Mwezi uliopita, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Benard Membe, wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuhusu maendeleo ya usuluhishi huo, alisema marais hao wastaafu walienda Malawi kukutana na Rais Joyce Banda na wiki iliyofuata wangekuja nchini.
Akizungumza na NIPASHE jana kwa njia ya simu, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano, wizarani hapo, Ally Mkumbwa, alisema Marais hao baada ya kuzungumza na Banda, hawatakuja nchini mpaka hapo watakapotoa taarifa kwa serikali hizo mbili ama kwenda Maputo, Msumbiji au wao wenyewe kwenda katika nchi hizo kwa ajili ya maendeleo ya usuluhishi huo.
Kwa mujibu wa Mkumbwa, Marais hao hawakutoa taarifa kwa wao kuahirisha kutokuja nchini kama ilivyolezwa hapo awali kwa kuwa ndio waliotoa taarifa ya safari yao na kwamba sio serikali hizo mbili ndizo zilizowaalika.
“Kwenda kwao nchini Malawi, yamkini ilikuwa kwa ajili ya kupata majibu zaidi kwa baadhi ya mambo fulani waliyoona hayajakaa vizuri kwenye taarifa kutoka nchini humo kwa ajili ya kuyafanyia uchambuzi kuhusiana na usuluhishi wa mgogoro huo,” alisema Mkumbwa na kuongeza:
“Kutokuja kwao huku ni kutokana na maamuzi yao wenyewe kwa kuwa sio sisi tuliowaita ila wao wenyewe ndio waliotoa taarifa ya kuja. Pia inawezekana kutokuja kwao kunatokana na kuridhika na taarifa zetu tulizowapelekea kwa upande wetu juu ya suala hilo, na hivyo kutoona umuhimu wa wao kuja tena.”
CHANZO: NIPASHE
No comments :
Post a Comment