Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Sunday, August 11, 2013

Sheikh Ponda adaiwa kupigwa risasi na Polisi

NA ASHTON BALAIGWA

11th August 2013


Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Nchini, Shekh Issa Ponda
Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Nchini, Shekh Issa Ponda, anadaiwa kupigwa risasi na kujeruhiwa begani wakati polisi wakiwa katika harakati ya kuwatawanya wafuasi wake waliokuwa wakimsindikiza kwa maandamano kuelekea katika msikiti wa Mungu Mmoja Dini Moja.
Inadaiwa kuwa alikuwa akitokea katika viwanja vya shule ya kiwanja cha ndege alikokuwa akihutubia kongamano.
Akiongea na gazeti hili, Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya kongamano hilo, Idd Mussa Msema alithibitisha Shekh Ponda amejuruhiwa kwa risasi begani wakati akisindikizwa na waandamanaji hao mara baada ya polisi kuvamia msafara huo wakati akielekea katika msikiti huo.
Tukio hilo lilitokea jana majira ya saa 12.25 jioni katika barabara ya Tumbaku mara baada ya kumalizika kwa mkutano wa kongamano lililoandaliwa na jumuiya ya wahadhiri wa kiislamu mkoa wa Morogoro.
Katika tukio hilo, inadaiwa kuwa shekhe Ponda aliyekuwa katika gari dogo, huku wafuasi wake wakimsindika kwa miguu, ndipo alipofika kwenye eneo la gereji mabomu ya machozi yalipigwa na polisi waliokuwa katika magari aina ya defender wakijaribu kuwatawanya wafuasi hao.
Baada ya tukio hilo, baadhi ya wafuasi walimchukua Shekh Ponda kutoka katika gari lake na kumkimbizia katika gereji moja, kisha wakatoka wakiwa wamempakia katika pikipiki na kumkimbiza katika hospitali ya Rufaa ya Morogoro.
Akizungumza hospitali hapo, Mlinzi mmoja wa lango namba moja alisema kuwa ulifika msururu wa pikipiki zaidi ya hamsini, lakini pikipiki zote zilizuiliwa isipokuwa iliyokuwa imembeba Shekh Ponda na kwenda naye mpaka mapokezi.
Aidha alisema wakiwa katika eneo hilo magari kadhaa ya polisi yaliingia katika lango la hospitali hiyo na hivyo wafuasi wa Shekh Ponda wakalazimika kumbeba begani na kuroka nae kupitia lango namba mbili.
Taarifa zilizopatikana baadaye zinadaiwa kuwa Shekh Ponda alikimbizwa katika hospitali nyingine ambayo haikufahamika .
Kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro, Faustine Shilogile akizungumzia tukio hilo, alidai kuwa mpaka kufikia majira ya saa 2.00 usiku hakuwa amepata taarifa zozote za kujeruhiwa kwa Shekh Ponda badala yake alidai kuwa amekuwa akisikia kwa watu waliokuwa wakimpigia simu.  
CHANZO: NIPASHE JUMAPILI

No comments :

Post a Comment