Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Sunday, August 11, 2013

Sheikh Ponda Issa Ponda apigwa risasi?

Sheikh Ponda Issa Ponda Katibu Mkuu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislam Tanzania
Sheikh Ponda Issa Ponda Katibu Mkuu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislam Tanzania
Kuna taarifa ambazo hazijathibitishwa na vyombo husika kuwa Shekh Ponda Issa Ponda amepigwa risasi na jeshi la polisi wakati akielekea msikitini  kwa ajili ya sala ya maghribi huko mkoani Morogoro.
Jeshi la Polisi mkoani Morogoro limekanusha kumpiga risasi Katibu wa Jumuiya ya Taasisi za Kiislam Sheikh Ponda Issa Ponda. Kamanda wa Polisi mkoani Morogoro ACP Faustine Shilogile amesema polisi walikwenda kumkamata lakini kwa kusaidiwa na wafuasi wake aliwatoroka na hawajui alipo. Jeshi hilo bado linamsaka na halina taarifa kama yupo hai au amekufa.
Kwa taarifa zilizopo hadi sasa Sheikh Ponda anaendelea vizuri na Imam wa msikiti wa Mtambani Sheikh Abdallah Suleiman amethibitisha kuwa Sheikh ni mzima na anaendelea vizuri anaomba hizi taaarifa za kumzushia kifo ziachwe mara moja.
Vile vile Sheikh Ponda alikosa huduma ya kwanza hospitali ya Morogoro kwa kuwa hakutimiza sharti ka kuwa kupata PF3 ya polisi ili apatiwe matibabu ya majeraha yake, chanzo cha karibu kimearifu kuwa wanaangalia uwezekano wa kumpatia matibabu kwengineko japo Sheikh amepoteza damu nyingi.
Chnazo: Zanzibari Yetu

No comments :

Post a Comment