dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Tuesday, October 22, 2013

Maalim Seif aonya vitambulisho vya ukaazi

NA MWANDISHI WETU

22nd October 2013


Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF),Maalim Seif Sharif Hamad
Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad amesema chama hicho kimedhamiria kuhakikisha kila Mzanzibari aliyetimiza umri wa miaka 18 anapata kitambulisho cha Mzanzibari Mkaazi (ZANID) ifikapo Julai mwakani.

Maalim Seif amesema hayo mwishoni mwa wiki iliyopita alipokuwa akihutubia wanachama wa chama hicho katika matawi na baraza mbalimbali wilaya ya Magharibi Unguja, akiwa katika ziara ya siku mbili kukagua uhai wa chama.

Alisema hayo baada ya kujitokeza malalamiko mengi kutoka kwa wanachama na wapenzi wa CUF wakidai wamekuwa wakinyimwa kwa makusudi vitambulisho hivyo kutokana na kile wanachoamini ni sababu za kisiasa.
Wanachama hao, katika majimbo ya Bububu, Mtoni, Mfenesini, na Dimani wamewatuhumu baadhi ya masheha kushirikiana na watendaji wa Ofisi ya Vitambulisho vya Mzanzibari Mkaazi, kuwanyima haki hiyo, ikiwamo baadhi yao kuzunguushwa licha ya kuwa na vyeti vya kuzaliwa.

Maalim Seif alisema uvumilivu mara zote una mwisho na kuwaonya wote wanaohusika na utoaji wa vitambulisho hivyo waache tabia hiyo, ili kuiepusha nchi kuingia kwenye matatizo.

“Uvumilivu mara zote una mwisho, msitusukume hadi tukafika ukutani, athari zake zinaweza kuwa mbaya kabisa,” alionya Maalim Seif.

Malalamiko hayo ya CUF yamekuja, licha ya kutolewa kauli na viongozi wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar akiwamo Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohammed Shein kuahidi kwamba wananchi wote wenye sifa watapatiwa vitambulisho hivyo.

CHANZO: NIPASHE

No comments :

Post a Comment