dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Wednesday, August 20, 2014

A CLARION CALL TO HELP KIVUNGE HOSPITAL IN ZANZIBAR!


Hi All,    
It is with sorrow and dismay to read about the state of affairs at Kivunge Hospital in Northern Zanzibar, as described here below by a staff writer of Maelezo Bi Fatma Kassim (August 18th, 2014). 


Bi Fatma writes that the hospital faces an enormous challenge when it comes to transferring expecting mothers and other emergency patients to the main referral hospital of Zanzibar, which is Mnazi Mmoja Hospital. 


According to the Chief Medical Doctor who is in charge of the hospital, the hospital is not offered enough funds for the purchase of gasoline for its only ambulance that was donated by the African Development Bank (ADB) in 2009.


The Chief Medical Doctor sadly narrates further that Zanzibar’s Ministry of Health budgeted to provide 400 litres of gasoline monthly to the hospital, but only a small portion of that amount is disbursed to the hospital, thereby hindering all the good efforts of the hospital in serving the people of Tumbatu, Matemwe and others from the Northern Region of Zanzibar.


Therefore, we at ZANZIBAR NI KWETU blog are making this clarion call to each and every one of us to come together and offer a helping hand to the hospital. We aim to raise at least 3,500 Canadian Dollars, so that the hospital could have a guarantee of at least 200 litres of gasoline per month for 12 months for emergency purposes. The 200 litres will be used only for the purpose of transferring patients who have emergency medical issues to the referral hospital, so that maternity and other deaths could be reduced at the hospital.


We do hope that the small contribution that we will accumulate online from good Samaritans, plus the little that the Ministry offers to the hospital monthly, will together somehow enable the hospital to extricate itself (even for one month) from the financial hardships that it is now wallowing in.

We ask all those who have been touched by the below article to donate generously for this humanitarian course.


May God help us to fulfill our desire to assist our brothers and sisters who are in need of our help. 

Ameen!


ZANZIBAR NI KWETU


                    HOSPITALI YA KIVUNGE YAOMBA USAFIRI
Na Fatma Kassim, Maelezo
Augosti 18, 2014.
"HOSPITALI ya Kivunge iliyopo Mkoa wa Kaskazini Unguja inakabiliwa na tatizo la usafiri wa wajawazito na wagonjwa wengine wanaohitaji huduma hiyo.

Wanaoathiriwa zaidi na tatizo hilo ni wale wanaopewa rufaa ya kwenda Hospitali Kuu ya Mnazimmoja kwa matibabu zaidi.

Daktari Dhamana wa Hospitali ya Kivunge, Dk. Shau Ali Hamdan alisema hospitali hiyo ina gari moja tu la kubebea wagonjwa ambalo hata hivyo linatumiwa kwa shughuli nyengine za kiofisi.

“Ni usumbufu mkubwa kwani linapotakiwa kubeba wagonjwa linakuwa katika shughuli zingine za ofisi na linapotakiwa kwa shughuli za ofisi linakuwa katika shughuli ya kubeba wagonjwa,” alisema na kulitaja gari hilo kuwa ni Ambulance.

Alisema pamoja na uwepo wa gari hilo, Dk Hamdan alisema wanakabiliwa na tatizo la mafuta ya kuendeshea gari hilo na inapotokezea mgonjwa kupatiwa rufaa, inamlazimu kuchangia shilingi 30, 000 kwa ajili ya mafuta.

Alisema Wizara ya Afya imepanga kuwapatia lita 400 za mafuta kila mwezi lakini hupatiwa chini ya kiwango hicho jambo linalokwamisha utekelezaji wa majukumuyao.Gari hiyo imetolewa kwa msaada wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (ADB) mwaka 2009 kwa ajili ya kuwahudumia wajawazito wanaopatiwa rufaa kupelekwa Hospitali kuu ya Mnazimmoja.

Dk. Hamdan alisema hospitali ya Kivunge inategemewa na wakaazi wa Mkoa wa Kaskazini Unguja wakiwemo wale wanaotoka mbali kama kisiwa cha Tumbatu, Kijijini Matemwe na sehemu nyengine.

Uwezo wa hospitali hiyo inapokea wastani wa wagonjwa 150 kwa siku, na wajawazito wanaohudumiwa kila mwezi wastani wa 250 na wanaopewa rufaa ni 22 kwa mwezi.

“Kuna baadhi ya wajawazito wanakuja moja kwa moja kujifungua hapa, lakini, wengine wanakuwa weshacheleweshwa, wengine wanakuja kwa kupatiwa rufaa na mara nyingi akifika hali ishakuwa mbaya, inabidi sisi tumpatie rufaa kwa kumuwahishia Mnazimmoja na hapo inabidi mgonjwa achangie mafuta”, alifahamisha Dk. Shau.

Wajawazito na wagonjwa wengine wanapopta rufaa kupelekwa Hospitali kuu ya Mnazimmoja wanapokosa usafiri hospitalini huwa wanatumia gari za kukodi ambazo hulazimika kulipia zaidi ya 30,000.

Dk. Hamdan alisema kutokana na hali hiyo, lengo la kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi litakuwa gumu kufikiwa iwapo mamlaka husika haitojipanga ipasavyo katika kuzipa kipaumbele huduma za mama wakati wa ujauzito wake, anapojifungua na baada ya kujifungua.

Wastani wa vifo vya wajawazito vinavyotokea kwa kila mwaka ni vinne katika hospitali hiyo.

Mkakati wa Kupunguza Umasikini Zanzibar (MKUZA), umelenga kupunguza vifo vya uzazi kutoka vifo 473 mwaka 2007 hadi vifo 170 kwa kila vizazi hai 100,000 ifikapo mwaka 2015.

Malengo ya Millenia namba tano ni kupunguza vifo vya uzazi kutoka 473 mwaka 2007 hadi 170 kwa kila vizazi hai 100,000 ifikapo mwaka 2015.

Katibu Mkuu Wizara ya Afya Zanzibar, Dk. Mohammed Saleh Jidawi, alisema, nia ya Wizara hiyo ni kutekeleza mikakati ya kuimarisha huduma za wajawazito katika hospitali pamoja na vituo vya afya huku wajawazito wakitakiwa kutochangia huduma wakati wa kujifungua".

http://www.zanzinews.com/2014/08/hospitali-ya-kivunge-yaomba-usafiri.html

                  http://www.gofundme.com/d74zjk

2 comments :

  1. Jamani tujitoleeni panapowezekana kwani unakuwa umeweka hazina mbinguni, Kutoa ni moyo jamani

    ReplyDelete
  2. Wala sio uwongo Da Amina hayo uyasemayo. Ukitoa leo basi hujapoteza, kwani utakuta kheri za hicho ulichokitua huko tuendako!

    ReplyDelete