dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Friday, August 29, 2014

Mhe Juma Duni amkabidhi majukumu ya Wizara ya afya Waziri mpya Rashid Seif

 Mkurugenzi Utumishi na Uendeshaji wa Wizara ya Afya, Juma Rajab Juma kulia akiwakaribisha Mawaziri wa Afya na Miundombinu katika hafla ya kukabidhiana Ofisi mawaziri hao baada ya kuteuliwa katika nafasi zao hivi karibuni.

 Aliyekuwa Waziri wa Afya ambaye kwa sasa ni Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano, Juma Duni Haji akizungumza na baadhi ya Watendaji wa Wizara ya Afya katika hafla ya kukabidhiana Ofisi iliyofanyika Wizara ya Afya Mnazi mmoja mjini Zanzibar.

 Aliyekuwa Waziri wa Afya ambaye kwa sasa ni Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano Juma Duni Haji akimkabidhi Ripoti Waziri mpya wa Wizara ya Afya Rashid Seif Suleiman katika hafla ya kukabidhiana Ofisi iliyofanyika ukumbi wa Wizara ya Afya Mnazi mmoja mjini Zanzibar.

Waziri wa Afya Rashid Seif Suleiman akizungumza na Watendaji wa Wizara hiyo mara baada ya kukabidhiwa Ofisi na Aliyekuwa Waziri wa Wizara hiyo Juma Duni Haji.Katika mazungumzo yake aliwaomba kushirikiana naye ili kutimiza malengo ya Wizara hiyo mpya kwake.
picha na Abdallah Omar-Maelezo Zanzibar
Chanzo: ZanziNews

No comments :

Post a Comment