dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Friday, March 6, 2015

Kilio hiki cha Nida ni fedheha kwa Serikali

Kwa hiyo, kilio cha sasa cha Nida kwamba haina fedha wala rasilimaliwatu ya kutosha kukabiliana na changamoto za kuandikisha wananchi nchini kinaonyesha matatizo tuliyoyaainisha karibu miaka miwili iliyopita.  
KWA UFUPI
Tangu 2013, hadi sasa tumesema katika safu hii kwamba mpango wa Serikali kuandikisha wananchi wake ili kuwapatia Vitambulisho vya Taifa hautafanikiwa endapo matatizo yaliyogubika mpango huo hayatapatiwa ufumbuzi wa kudumu.
Kilio cha sasa cha Wakala wa Vitambulisho vya Taifa (Nida) kwamba hawana fedha wala wafanyakazi wa kutosha, siyo kipya kwenye masikio ya Watanzania.
Tangu 2013, hadi sasa tumesema katika safu hii kwamba mpango wa Serikali kuandikisha wananchi wake ili kuwapatia Vitambulisho vya Taifa hautafanikiwa endapo matatizo yaliyogubika mpango huo hayatapatiwa ufumbuzi wa kudumu.
Tulisema baada ya uchunguzi wetu mikoani kuwa utekelezaji wa mpango huo haukufanyiwa matayarisho ya kutosha, ikiwa ni pamoja na Serikali kushindwa kutoa fedha za kutosha na kwa wakati na watekelezaji wake hawakuandaliwa vya kutosha au waliendesha mambo kwa mazoea.
Isitoshe, yapo madai ya msuguano wa chini kwa chini kati ya Nida na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec), kutokana na kila kimoja kutaka kupewa kipaumbele na Serikali katika kupewa fedha kwa vyombo hivyo vinafanya kazi zinazofanana.
Tulishauri kuwa ingekuwa vyema ikateuliwa taasisi mojawapo itayarishe vitambulisho vya kupiga kura na vya uraia.
Uchunguzi wetu Julai mwaka juzi ambao una mashiko leo unaonyesha kusuasua kwa mpango huo, kwa maana kwamba wananchi wengi mijini na vijijini wameshindwa kujiandikisha, wengine majina yao hayakutokea, ama yamekosewa.
Kwa hiyo, kilio cha sasa cha Nida kwamba haina fedha wala rasilimaliwatu ya kutosha kukabiliana na changamoto za kuandikisha wananchi nchini kinaonyesha matatizo tuliyoyaainisha karibu miaka miwili iliyopita.
Tulieleza wakati ule kuwa matatizo hayo ndiyo yaliyokwamisha uandikishaji, tukasema kuwa tatizo kubwa ni Serikali kutofahamu nini kinaendelea katika mchakato mzima wa uandikishaji, kwa maana ya kutosimamia au kufuatilia utekelezaji wake.
Tunasema, pamoja na kilio hicho cha sasa cha ukosefu wa fedha na rasilimaliwatu, Nida lazima ikiri waandikishaji wake tangu awali walipaswa kupewa mafunzo stahiki ili kuepusha makosa na ubabaishaji ulioshuhudiwa kila mahali ulikofanyika uandikishaji, uhakiki wa majina na kutoa vitambulisho.
Kwa mfano, tumeshuhudia misururu mirefu ya wananchi wakihakiki majina yao kwenye baadhi ya maeneo jijini Dar es Salaam siku chache zilizopita, ambako adha ilikuwa kubwa kupindukia. Tunassema maofisa wa Nida wajitazame upya viwango vyao kiutendaji na inawezekana elimu yao.
Kama tulivyoeleza awali, Nida na Nec wanafanya kazi inayofanana, wote wanalia njaa, hawana fedha na hiyo ni fedheha kwa Serikali.
Nec, wanaosimamia uandikishaji kwenye daftari la kudumu la wapigakura kule mkoani Njombe, wamekuwa wakilia kwa ukosefu wa fedha na vifaa kufanikisha kazi hiyo. Kilio hicho kilipomfikia Rais Jakaya Kikwete aliagiza fedha zinazopatikana kwenye makusanyo ya kodi, zipelekwe Nec ili kufanikisha uandikishaji.
Inawezekana, Nida wametoka hadharani na kueleza mambo yanayowasibu kwa sasa, wamejiepusha na lawama zinazoendelea kujitokeza kwao, ukiwamo udhaifu mkubwa kwenye utoaji wa vitambulisho hata kwenye maeneo ambako uandikishaji umefanyika na kukamilika.
Ni kama tulivyoeleza awali, Nida ilishindwa kuendesha programu kubwa ya uhamasishaji kwa kutoa elimu ya kutosha kwa wananchi kupitia vyombo vya habari. Tunasema, Nida ilichelewa kueleza matatizo ya ukata yanayoisibu na kuifanya hadi sasa iwe imeandikisha Watanzania wachache ikilinganishwa na muda iliotumia.

No comments :

Post a Comment