dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Sunday, April 26, 2015

Moyo: Sijutii kutimuliwa ndani ya CCM

Image result for hassan nassor moyo


Muasisi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Hassan Nassor Moyo (pichani), aliyetimuliwa kutoka kwenye chama hicho wiki iliyipita, amesema hajutii kufukuzwa na wala hajaathirika kwa lolote.

Moyo alivuliwa uanachama na Halmashauri ya Mkoa wa Mjini Magharibi kwa madai kuwa alikuwa  msaliti ndani ya  chama.

Akizungumza na  NIPASHE mara baada ya kutilimuliwa kwenye chama hicho, Moyo alisema suala la vyama ni jambo la mpito, hivyo hajutii kufukuzwa kwake.

Moyo ambaye pia alikuwa muasisi wa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, alisema madai kwamba anakisaliti Chama cha CCM ni mitazamo ya watu wasioitakia mema Zanzibar.

“Mimi nilichokuwa nakifanya ni kutetea maslahi ya Zanzibar, kufanya hivyo ndiyo kukisaliti chama?”,  alihoji. 

Hata hivyo, alisema uamuzi huo wa kumfukuza kwenye chama chake hautamteteresha wala kumzuia kuitetea Zanzibar kuwa na mamlaka kamili.
Moyo mara kwa mara amekuwa akidaiwa kupinga muundo wa serikali mbili na kutetea muundo wa serikali tatu, katika suala la Muungano.NIPASHE ilizungumza na wazee mbalimbali, visiwani hapa ambao, walisema wamepongeza hatua ya Halmahauri  hiyo ya kumvua uanachama Moyo, wakidai kuwa ni msaliti wa Muungano.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti, walidai kuwa Moyo amekuwa akikiuka maadili ya CCM kila mara.Wajumbe wa Baraza la Wazee wa CCM, walisema ni uamuzi sahihi ambao unakwenda katika kusimamia maadili, Katiba ya chama na sera zake.

Muasisi wa Mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 1964, Hamid Ameir, alisema kwa muda mrefu wamekuwa wakisikitishwa na uamuzi wa mzee Moyo wa kutoa kauli mbalimbali zinazokwenda kinyume na Sera na Katiba ya chama.

Alisema muasisi huyo amekuwa akipinga muundo wa Muungano wa serikali mbili ambao amekuwa akiutumikia.

"Sisi wazee tunaunga mkono uamuzi wa halmahauri ya mkoa wa Mjini Magharibi wa kumvua uanachama wa Chama Cha Mapinduzi mzee Moyo, kwa sababu amekuwa msaliti ndani ya chama kwa kujiunga katika chama cha CUF na kupanda katika majukwaa ya kisiasa akitukana serikali ambayo ameitumikia kwa muda mrefu," alisema.

Haji Simai, alisema wamefurahishwa na uamuzi huo kwa sababu tayari mzee Moyo alikuwa amekisaliti chama chake kwa kukikejeli hadharani na kukifananisha na chama kilichopitwa na wakati.

'Sisi wanachama wa Chama Cha Mapinduzi tumekuwa tukifuatilia mikutano ya CUF ambayo amekuwa akialikwa mzee Moyo, kauli zake dhidi ya CCM pamoja na Muungano zinaonesha dhahiri kwamba tayari amejivua uanachama kwa muda mrefu," alisema.

Amina Iddi, mjumbe wa wazee wa CCM alisema chama chao kimemvumilia kwa muda mrefu mzee Moyo kwa kutukana waasisi ambao wao ndiyo waliompa madaraka makubwa ya kushika nyadhifa mbalimbali serikalini ikiwamo Zanzibar na Muungano.

"Huyu mzee amevumiliwa sana kwa kutoa kauli za matusi na kebehi ikiwamo kuwakashifu viongozi walioleta Muungano wakati yeye kwa muda wa maisha yake yote ameutumikia kwa nguvu zote," alisema.

Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Chama cha CUF, Salim Bimani, alisema uamuzi wa kumfukuza mzee Moyo kutoka CCM haukuwa sahihi kwa sababu ni mtu mwenye busara, hekima na uwezo mkubwa.

Bimani alisema kitendo cha CCM kumfukuza muasisi huyo ni kuchanganyikiwa kisiasa.

“Wazee kama wale ambao wana hekima na busara wanahitaji kuenziwa kwani ni wazee wa kitaifa,” alisema Bimani.
CHANZO: NIPASHE JUMAPILI

No comments :

Post a Comment