dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Sunday, April 12, 2015

ZEC yaombwa kutoa ripoti ya ugawaji majimbo

Image result for ZANZIBAR ELECTION COMMISSION


Wadau wa uchaguzi Zanzibar wameiomba Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), kuharakisha utoaji wa ripoti ya ugawaji wa majimbo ili vyama vya siasa viweze kujiandaa na Uchaguzi Mkuu ujao.

Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Vuai Ali Vuai, alisema hayo wakati akitoa maoni yake katika mkutano wa wadau wa uchaguzi kuhusu maandalizi ya oboreshaji wa Daftari la Wapiga Kura, unaotarajiwa kuanza wiki ijayo.

Vuai alisema chama chake kinasubiri kwa hamu ripoti hiyo kwani wanashindwa kujipanga  ikiwamo suala la kutafuta wagombea wa nafasi mbalimbali za uchaguzi kupitia chama hicho.

Aliishauri Tume hiyo kuangalia kwa makini vigezo vya ugawaji wa majimbo ili haki iweze kutendeka, hasa suala la idadi ya watu kwani baadhi ya wilaya Zanzibar zina idadi kubwa ya watu wakati majimbo ni machache.

Vuai alitoa mfano Wilaya ya Magharibi ambayo ina majimbo tisa wakati idadi ya watu ni zaidi ya 350,000 wakati wilaya zote za Pemba zina majimbo 18  na idadi ya watu ni 400,000.

Rashid Mchenga kutoka chama cha Tadea, alishauri kuwa ripoti ya ugawaji wa majimbo kuharakishwa na kuitaka Tume hiyo kuwatoa kwenye daftari la wapiga kura watu ambao wameshafariki dunia.

Laila Abdallah Masoud, aliitaka Tume hiyo kuweka utaratibu mzuri wa watu wenye ulemavu na wazee wasiojiweza kushiriki katika zoezi la kujiandikisha bila ya kupata usumbufu.

Akizungumzia uchunguzi wa mipaka ya majimbo ya uchaguzi, Mwenyekiti wa ZEC, Jecha Salim Jecha, alisema Tume hiyo  imeshakamilisha uchambuzi wa maoni na iko katika hatua ya mwisho ya utayarishaji wa ripoti ya kazi husika ili iweze kuwasilishwa kwa wadau wa uchaguzi.
CHANZO: NIPASHE JUMAPILI

No comments :

Post a Comment