dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Sunday, May 3, 2015

Uzinduzi wa Mfuko wa Uchaguzi wa Mkoa wa Magharibi Kichama.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo  Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Waziri Mkuu wa Tanzania Mizengo Pinda jana wakati wa Uzinduzi wa mfuko wa Uchaguzi wa Mkoa wa Magharibi Kichama uliofanyika ukumbi wa Hotel Zanzibar Beach Resort,
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar alipokuwa akitoa nasaha zake kwa wanachama na wapenzi wa CCM  wakati wa uzinduzi wa Mfuko wa uchaguzi wa Mkoa wa Magharibi,Kichama uliofanyika jana katika ukumbi wa Hoteli ya Zanzibar Beach Resort Nje ya Mji wa Unguja
Baadhi ya WanaCCM na Wakereketwa na Viongozi wakiwa katika hafla ya uzinduzi wa Mfuko wa uchaguzi wa Mkoa wa Magharibi,Kichama uliofanyika jana katika ukumbi wa Hoteli ya Zanzibar Beach Resort Nje ya Mji wa Unguja
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar akimkabidhi Mwenyekiti wa wa Vijana Wilaya ya Mfenesini Marakibu Mbarouk Mrakibu Picha ya kuchora ya kukabidhiana hati ya Muungano Mzee Karume na Mwalimu Nyerere iliyouzwa kwa mnada Shilingi MIllioni Ishirini na Tatu wakati wa uzinduzi wa Mfuko wa uchaguzi wa Mkoa wa Magharibi,Kichama uliofanyika jana katika ukumbi wa Hoteli ya Zanzibar Beach Resort Nje ya Mji wa Unguja (kushoto) Waziri Mkuu wa Tanzania Mizengo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar akimkabidhi Abdulghafar Idrissa Mikoba ya Ukili iliyouzwa kwa mnada wa shilingi Milioni Mbili wakati wa uzinduzi wa Mfuko wa uchaguzi wa Mkoa wa Magharibi,Kichama uliofanyika jana katika ukumbi wa Hoteli ya Zanzibar Beach Resort Nje ya Mji wa Unguja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo  Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) Waziri Mkuu wa Tanzania Mizengo Pinda(wa pili kushoto) Waziri Kiongozi Mstaafu Shamsi Vuai Nahodha(kushoto) Mama Mwanamwema Shein (kulia) na Mwenyekiti wa Mkoa wa Magharibi Yussuf Mohammed Yussuf wakiwa katika hafla ya  Uzinduzi wa mfuko  wa Uchaguzi wa Mkoa wa Magharibi Kichama uliofanyika ukumbi wa Hotel Zanzibar Beach Resort jana,
Kikundi cha Imarisha cha CCM MKoa Amani kikitoa burudani ya ngoma ya Tukulanga wakati wa Uzinduzi wa mfuko  wa Uchaguzi wa Mkoa wa Magharibi Kichama uliofanyika jana katika ukumbi wa Hotel Zanzibar Beach Resort mgeni rasmi akiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo  Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein
Mtoto wa Marehemu Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere, Makongoro Nyerere akipokea  picha ya Mzee Karume na Mwalimu Nyerere wakikagua gwaride kutoka kwa  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo  Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein iliyouzwa kwa mnada shilingi Millioni Nne wakati waUzinduzi wa mfuko  wa Uchaguzi wa Mkoa wa Magharibi Kichama uliofanyika ukumbi wa Hotel Zanzibar Beach Resort jana
Picha ya kuchora ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein ikiwa katika mnada kwa wanachama na wafanyabiashara mbali mbali wakati wa Uzinduzi wa mfuko  wa Uchaguzi wa Mkoa wa Magharibi Kichama uliofanyika jana katika ukumbi wa Hotel Zanzibar Beach Resort iliyouzwa kwa shilingi millioni Ishirini na Tatu na Laki mbili
Baadhi ya Viongozi waliohudhuria katika Uzinduzi wa mfuko wa Uchaguzi wa Mkoa wa Magharibi Kichama uliofanyika jana katika ukumbi wa Hotel Zanzibar Beach Resort akiwepo Mke wa Mamako wa Pili wa Rais Mama Pili Balozi Seif Ali Iddi (wa pili kushoto)
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo  Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akipokea taarifa kutoka kwa Katibu wa CCM Mkoa wa Magharibi Aziza Mapuri jana wakati waUzinduzi wa mfuko  wa Uchaguzi wa Mkoa wa Magharibi Kichama uliofanyika ukumbi wa Hotel Zanzibar Beach Resort jana
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo  Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akipokea mchango wa fedha tasilim shilingi Millioni Nne  kutoka kwa Waziri asiyekuwa na Wizara maalu na Mjumbe wa Halamashauri Kuu ya CCM NEC Machano Othman Said wakati wa Uzinduzi wa mfuko wa Uchaguzi wa Mkoa wa Magharibi Kichama uliofanyika jana katika ukumbi wa Hotel Zanzibar Beach Resort
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo  Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akipokea mchango wa fedha tasilim shilingi Millioni Tano kutoka kwa Waziri wa Fedha Omar Yussuf na Mkewe wakati wa Uzinduzi wa mfuko  wa Uchaguzi wa Mkoa wa Magharibi Kichama uliofanyika jana katika ukumbi wa Hotel Zanzibar Beach Resort. 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo  Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akipokea mchango wa fedha tasilim na Cheki  kutoka kwa Mfanyabiashara Ahmada Shaa   wakati wa Uzinduzi wa mfuko  wa Uchaguzi wa Mkoa wa Magharibi Kichama uliofanyika jana katika ukumbi wa Hotel Zanzibar Beach Resort
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo  Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akipokea mchango wa fedha tasilim shilingi Millioni tano kutoka kwa Mwakilishi wa Kampuni ya kuuza Kuu (Peduu) Issa Kassim Issa wakati wa Uzinduzi wa mfuko  wa Uchaguzi wa Mkoa wa Magharibi Kichama uliofanyika jana katika ukumbi wa Hotel Zanzibar Beach Resor
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo  Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akipokea mchango wa fedha tasilim kutoka kwa Mwenyekiti wa Umoja wa Wazazi Tanzania Abdalla Bulembo  wakati wa Uzinduzi wa mfuko  wa Uchaguzi wa Mkoa wa Magharibi Kichama uliofanyika jana katika ukumbi wa Hotel Zanzibar Beach Resort
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo  Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akipokea mchango wa fedha sillingi milioni mbili na nusu kutoka kwa Tauhida Cassiun Galos Nyimbo Mbunge CCM wakati wa Uzinduzi wa mfuko  wa Uchaguzi wa Mkoa wa Magharibi Kichama uliofanyika ukumbi wa Hotel Zanzibar Beach Resort jana
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo  Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akipokea mchango wa fedha tasilim shilingi Millioni Mbili na Nusu kutoka kwa Mwakilishi wa Jimbo la Bububu Ibrahim Hussein Makungu (Bhaa) wakati wa Uzinduzi wa mfuko  wa Uchaguzi wa Mkoa wa Magharibi Kichama uliofanyika jana katika ukumbi wa Hotel Zanzibar Beach Resort
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo  Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akipokea mchango wa fedha tasilim shilingi Millioni Moja kutoka kwa Mjumbe wa Kamati Kuu wa CCM Khadija Mohamed Aboud Uzinduzi wa mfuko  wa Uchaguzi wa Mkoa wa Magharibi Kichama uliofanyika jana katika ukumbi wa Hotel Zanzibar Beach Resort
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo  Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akimkabidhi Waziri wa Fedha na Mjumbe wa halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM NEC Omar Yussuf Mzee vyeti vya Shukurani kwa wafanyabishara na Wanachama mbali mbali waliochangia fedha   wakati waUzinduzi wa mfuko  wa Uchaguzi wa Mkoa wa Magharibi Kichama uliofanyika ukumbi wa Hotel Zanzibar Beach Resort jana
Mke wa Rais wa zanzibar Mama Mwanamwema Shein akimkabidhi keki MkuuKiongozi wa  Kikundi Imarisha cha CCM Mkoa Amani Marium Omar keki iliyonadishwa kwa Shillingi Millioni Kumi na Mbili wakati wa Uzinduzi wa mfuko wa Uchaguzi wa Mkoa wa Magharibi Kichama uliofanyika ukumbi wa Hotel Zanzibar Beach Resort jana
Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein (katikati) akishikilia Keki akiwa na Wajumbe waliochangia keki hiyo iliyouzwa kwa mnada wa shilingi Milioni Kumi na Mbili wakati wa mchango maalum wakati wauzinduzi wa Mfuko wa uchaguzi wa Mkoa wa Magharibi,Kichama uliofanyika jana katika ukumbi wa Hoteli ya Zanzibar Beach Resort Nje ya Mji wa Unguja
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar pamja na Viongozi wengine (katikati) wakiwa katika Picha ya Pamoja na wanakamati wa Ushuhulikiaji uchagishaji Mfuko wa Uchaguzi wa Mkoa wa Magharibi,Kichama uliofanyika jana katika ukumbi wa Hoteli ya Zanzibar Beach Resort Nje ya Mji wa Unguja,[Picha na Ikulu.]

Dk Shein: Moyo wa Kujitolea Umeiwezesha CCM Kutekeleza Malengo yake Inayojiwekea.

STATE HOUSE ZANZIBAR

OFFICE OF THE PRESS SECRETARY
PRESS RELEASE
    Zanzibar                                                             02 Mei, 2015
---
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein amewapongeza wanachama na wapenzi wa Chama cha Mapinduzi kwa moyo wao wa kujitolea ambao daima umekiwezesha chama hicho kutekeleza malengo yake iliyojiwekea.
Akizungumza katika harambee ya kuchangia chama hicho Mkoa wa Magharibi –kichama iliyofanyika katika hoteli ya Zanzibar Beach Resort mjini Unguja jana, Dk. Shein alisema amefurahishwa na ari na moyo waliokuwa nao washiriki wa harambee hiyo ambapo ilikiwezesha chama hicho kukusanya jumla ya shilingi milioni 644.54.
 Aliipongeza Kamati ya Maandalizi ya Harambee hiyo pamoja na viongozi wa Chama hicho mkoa sio tu kwa maandalizi mazuri lakini pia kwa wao wenyewe kujiwekea utaratibu wa kuchangia harambee hiyo jambo ambalo limewahamasisha wachangiaji wengine.
Dk. Shein aliwashukuru wageni mbalimbali waliohudhuria hafla hiyo wakiwemo wanachama na wapenzi wa CCM pamoja na wafanyabiashara mbalimbali wa hapa Zanzibar na Tanzania Bara.
Aliwaeleza wana CCM na wageni waliohudhuria hafla hiyo kuwa alikuwa na hakika wakati alipotoa rai kwa viongozi wa CCM tarehe 24 Aprili, 2013 kufanya harambee kuchangia maendeleo ya chama hicho kuwa  zoezi hilo litafanikiwa.
Hadi sasa mikoa iliyokwishafanya harambee hizo ni mikoa ya yote ya kichama ya Unguja ambayo ni Kaskazini, Kusini, Mjini na Mkoa wa Magharibi.
Kati ya fedha zilizokusanywa, shilingi 120.7 zilikuwa fedha taslim, milioni 490.8 ahadi na hundi ilikuwa shilingi milioni 33.
Dk. Shein alichangia shilingi milioni 15 wakati Mke wake Mama Mwanamwema Shein alichangia shilingi milioni 5.
Miongoni mwa wachangiaji walikuwa ni pamoja na Waziri Mkuu wa zamani Mheshimiwa Edward Lowasa milioni 50, Kampuni ya Simon Group shilingi milioni 30, Kampuni ya ujenzi ya MECCO shilingi milioni 20 na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mheshimiwa Benard Membe milioni 10.
 Katika harambee hiyo marafiki wa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Mizengo Peter Pinda waliahidi mchango wa shilingi milioni 203 wakati yeye mwenywe alichangia shilingi milioni 10.
 Akizungumza katika hafla hiyo, Waziri Mkuu Pinda alisema ari iliyooneshwa katika harambee hiyo inadhihirisha msemo wa ‘kutoa ni moyo si utajiri’.
 Alisifu ari ya washiriki wa hafla hiyo na kueleza kuwa ilikuwa ya hali ya juu na yeye binafsi ametiwa moyo sana na kitendo hicho cha wana CCM katika harambee hiyo.
 Katika hafla hiyo vitu mbalimbali vya asili pamoja na picha za kumbukumbu za kitaifa zilinadiwa na kununuliwa kwa fedha nyingi ikiwemo picha ya kuchora ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Shein ambayo ilinunuliwa kwa shilingi milioni 23.
 Kitu kingine kilichovutia katika mnada ni keki yenye rangi ya Chama cha Mapinduzi ambayo mnada wake ulishamirishwa na Mke wa Rais Mama Mwanamwema Shein na hatimae kununuliwa kwa shilingi milioni12.  


Postal Address: 2422 Tel.+255 776 613 015, Fax: 024 2231822 


No comments :

Post a Comment