dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Thursday, June 25, 2015

CCM yalaani mawaziri CUF kutoka barazani

Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Vuai Ali Vuai.
Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar, kimesema kimesikitishwa sana na kitendo cha wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kutoka Chama cha Wananchi (CUF) kususia kikao cha Baraza la Wawakilishi hasa mawaziri kutoka chama hicho kwani nao ni miongoni mwa viongozi katika Serikali ya Umoja wa Kitaifa.
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Vuai Ali Vuai, alisema kitendo hicho cha wajumbe hao hasa mawaziri ni kitendo kibaya na ni kumdhalilisha rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein.
Alisema CCM kimeshangaa na hawakutarajia kitendo hicho kutokea hasa ikizingatiwa kuwa CCM na CUF wamekubaliana na kuunda serikali ya umoja wa kitaifa.
“Kilichotushtua ni mawaziri kutoka CUF kuungana na wajumbe wezao kususia kikao kwa lengo la kukwamisha muswada wa sheria wa kuidhinisha matumizi ya fedha za bajeti na kama mswada huo ungeshindwa kupitishwa serikali ingeshindwa kufanya mambo yake ya msingi,” alisema Vuai.
Aliongeza: ”Kitendo kile sisi tunakiita ni vichekesho na vituko kwani inaonyesha dhahiri yale mapenzi ya CCM kuungana nao na kupatikana kwa SUK ili kuondokana na siasa za chuki na uhasama,  wezetu  tunaona hawataki hivyo na sisi tutafikiria,” alisema. “Walichokifanya wezetu hawa ni ubakaji wa kidemokrasia na unafiki wa kisiasa kwanini wasitoke mwanzo wa vikao vya bajeti vilipoanza na kuamua kutoka ukingoni ambapo zimebaki siku tatu tu rais kuvunja baraza hilo?” Vuai.
CHANZO: NIPASHE

No comments :

Post a Comment