dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Saturday, June 27, 2015

Dk. Shein afunga Baraza la Wawakilishi bila wajumbe CUF.

Rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohammed Shein.
Rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohammed Shein jana ameufunga rasmi mkutano wa nane wa baraza la wawakilishi huku kukiwa hakuna hata wajumbe na mawaziri kutoka chama cha wananchi CUF, waliosusia vikao vya baraza hilo.
Akiwahutubia wajumbe wa baraza hilo kutoka CCM na wageni waalikwa huko Chukwani, nje kidogo ya mji wa Zanzibar, alisema kila mmoja anaelewa kwamba Baraza hilo linaendeshwa kwa misingi ya Sheria na Kanuni.
Alisema wakati Wajumbe wa Baraza hilo kutoka chama cha CUF waliposusia kikao cha baraza hilo mwanzoni mwa wiki hii, hoja walizozitoa ambazo hawakuridhishwa na uwandikishaji wa daftari la wapiga kura wapya, hazikuwa na mnasaba na hoja iliyokuwa imewasilishwa ndani ya baraza hilo ili ijadiliwe.
“Siku hiyo Waziri wa Fedha alikuwa amewasilisha hoja ya kujadiliwa kwa Muswada wa Sheria ya Matumizi ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2015/2016 ambao haukuwa na uhusiano hata kidogo na masuala ya kujiandikisha katika daftari la kudumu la kupiga kura,” alisema Dk Shein.
Alisema kuwa hoja ya wajumbe hao wa CUF inahusiana na Sheria nyingine, ambayo ni Sheria ya Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar, namba 9 ya mwaka 1992 inayosimamiwa na Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar pamoja na Sheria ya Usajili wa Mzanzibari Mkaazi, namba 7 ya mwaka 2005.
Aidha alisema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itaendelea kuhakikisha kila mwananchi mwenye sifa ya kupiga kura anapewa haki yake na kuwataka wanasiasa wasiwapotoshe wananchi juu ya haki yao hiyo.
AMANI NA USALAMA
Dk. Shein akizungumzia hali ya amani na usalama alisema, siri kubwa ya mafanikio ya nchi katika sekta zote za maendeleo ni kuendelea kuimarika kwa hali ya amani na utulivu nchini.
Alisema katika kipindi chote cha miaka mitano, Idara maalum za SMZ, Serikali ya Zanzibar na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania vimetekeleza vyema jukumu lao la kusimamia ulinzi, amani na utulivu kwa kuhakikisha maisha ya watu na mali zao yamekuwa salama.
MUUNGANO.
Akizungumzia Muungano wa Tanganyika na Zanzibar Dk. Shein, alisema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Awamu ya Saba inatambua na inazingatia haja ya kuimarisha Muungano wa Tanzania kama nguzo ya pili muhimu baada ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar ya mwaka 1964 kwa malengo yale yale ya waasisi wa Muungano huo.
Alisema ni dhahiri kuwa nguzo hizo za Mapinduzi na Muungano ndizo zimewezesha kupiga hatua kubwa za maendeleo kisiasa, kiuchumi na kijamii na kuleta heshima ya Wazanzibari na Watanzania mbele ya mataifa mbali mbali katika kipindi cha miaka 51.
Alisema katika kipindi hiki cha miaka mitano, Muungano huo umezidi kuimarika kutokana na hatua zinazochukuliwa na viongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
UCHIMBAJI WA MAFUTA NA GESI
Alisema amefurahi kuona kuwa  Baraza hilo la Nane limejadili kwa kina suala la uchimbaji wa mafuta na gesi na limeweza kutoa michango na kuishauri serikali kwa namna mbali mbali kuhusiana na suala hilo. Alisema hivi sasa wamefikia pazuri hasa ikizingatia kuwa Katiba inayopendekezwa imezingatia matakwa ya Zanzibar juu ya suala hilo.
CHANZO: NIPASHE

No comments :

Post a Comment