dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Friday, September 4, 2015

Masaburi aibuka sakata la vijana kuandamana.

  Polisi wafanya upelelezi kubaini ni wa chama gani.

Mgombea Ubunge Jimbo la Ubungo kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Dk. Didas Masaburi.
Mgombea Ubunge Jimbo la Ubungo kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Dk. Didas Masaburi (pichani), amekanusha taarifa za kufadhili vijana wanaodaiwa kuandamana wakipinga aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kuondoka ndani ya chama hicho. 
 
Dk. Masaburi alikanusha taarifa hizo jana wakati akizungumza na  waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuhusiana na uvumi uliozagaa kwenye mitandao ya jamii kuwa vijana 10 wanaoshikiliwa na Jeshi la Polisi kwa sababu ya kuandamana bila ya kibali wakimtaka Dk. Slaa asiondoke kwenye chama hicho walitumwa na yeye.
 
“Tuhuma hizo si za kweli, hata kama ninaunga mkono hoja zilizotolewa na Dk. Slaa kuhusiana na tuhuma za ufisadi dhidi ya viongozi waliohamia Chadema kutoka CCM, lakini siwezi kufadhili maandamano ya wanachama wa Chadema ya kushinikiza  kubakia kwa Dk. Slaa ndani ya chama hicho,” alisema.
 
Alisema vijana aliowapokea katika ofisi ya CCM Jimbo la Ubungo zilizoko Manzese juzi baada ya kurudisha kadi za vyama vyao kikiwamo cha Chadema walifanya hivyo kwa mapenzi yao wakisema wamechoshwa na hadaa katika vyama walivyotoka. Aidha, Dk. Masaburi aliwataka viongozi wa Chadema kujibu hoja zilizotolewa na Dk. Slaa badala ya kutafuta mchawi baada ya kuona amewaumbua na wanachama wao wanakihama chama hicho.Wakati huohuo, Jeshi la Polisi mkoa wa Kinondoni, jijini Dar es Salaam limesema linaendelea na upelelezi ili kubaini vijana walioandamana juzi eneo la Morocco, jijini humo iwapo ni wanachama wa Chadema au  la.
 Juzi vijana takribani 100 wanaodaiwa kuwa wanachama wa Chadema waliandamana katika eneo hilo wakishinikiza kurudi katika chama hicho kwa aliyekuwa  katibu mkuu wake, Dk. Willibrod Slaa, ambaye alitangaza kujitoa na kujitenga na siasa, huku  akimtuhumu mgombea urais wa chama hicho, Edward Lowassa, masuala mbalimbali ua ufisadi.
 
Kamanda wa Polisi wa kanda ya Kinondoni, Camilius Wambura kupita msaidizi wake, jana aliliambia Nipashe kuwa bado wanawashikilia vijana 10 kati ya 100 ambao walitawanywa kwa mabomu ya machozi baada ya kukaidi amri ya jeshi hilo ya kutakiwa kutawanyika, huku wakiendelea na upelelezi kubaini wanatoka chama gani.
CHANZO: NIPASHE

No comments :

Post a Comment