dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Wednesday, October 21, 2015

Jinsi ya kutambua kura zilizoharibika, halali!



Elimu ya Mpigakura 
By Julius Mathias, Mwananchi
Dar es Salaam. Jumapili ni siku muhimu ya kuhitimisha harakati za kisiasa zilizodumu kwa takribani miezi sita ikijumuisha kutangaza nia, kuchukua fomu, kutafuta wadhamini, uteuzi ndani ya vyama mpaka kampeni za majukwaani. Kufanikisha hilo, unatakiwa kufahamu yafuatayo:
Kura iliyoharibika ni ile ambayo;
1. Haina alama yoyote.
2. Imepigwa kwa wagombea zaidi ya mmoja,
3. Imeandikwa jina la mpiga kura,
4. Alama imewekwa nje ya kisanduku cha picha
ya mgombea
5. Haina muhuri wenye alama rasmi
Kura sahihi;
1. Yenye alama ya ‘v’ kwenye kisanduku.
2. Yenye alama yoyote kwenye kisanduku/picha/ jina la mgombea.
Kutakuwa na utata endapo utaweka alama iliyopitiliza kisanduku cha mgombea mmoja na kufika kwa
mwingine. Epuka kuharibu kura. Kura yako, mustakabali wako.

No comments :

Post a Comment