dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Thursday, October 22, 2015

Kubenea aipa angalizo Nec.

Mgombea ubunge wa Jimbo la Ubungo kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Saeed Kubenea.
Mgombea ubunge wa Jimbo la Ubungo kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Saeed Kubenea (pichani), ameitaka Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec), kuhakikisha wapigakura wote watakaopiga kura wanakidhi vigezo na si ‘feki’. Aidha, amewatahadharisha viongozi na wasimamizi ambao watakuwa chanzo cha vurugu na kushindwa kusimamia majukumu yao kujihadhari na Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC).
 
Akihutubia mkutano wa kampeni za uchaguzi katika viwanja vya TP Manzese jijini Dar es Salaam juzi, Kubenea alisema Chadema itakapoingia madarakani italeta mabadiliko kwa maisha ya Watanzania katika huduma zote za kijamii.“Nasema serikali ya CCM imeshindwa kuheshimu raia wake kwa kuwapa huduma bora za afya, dereva wa bodaboda akipata ajali matibabu ni tatizo na kuna msongamano Moi, mtuchague Chadema tutawaheshimu Watanzania,” alisema Kubenea. 
 
Alisema CCM imefikia mwisho wa kuwaongoza Watanzania, hivyo kupitia uchaguzi huu, wapigakura waing’oe madarakani.
 
Naye Mwenyekiti wa Chadema Sinza, Leonce Barongo, alisema zaidi ya bodaboda 3,000 aina ya Yamaha ambazo kila moja itauzwa Sh. milioni 2.3, zitatolewa kwa mkopo usio na riba kwa wakazi wa Jimbo la Ubungo na maeneo mengine, ili kuwasaidia kujiajiri wenyewe. Alisema tayari bodaboda hizo zimeanza kutolewa kwa wakazi wa jimbo hilo pamoja na wale wote ambao wametimiza masharti ya kuwa na akaunti benki sambamba na barua ya kutambuliwa mahali anakoishi.
CHANZO: NIPASHE

No comments :

Post a Comment