dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Wednesday, October 14, 2015

Lowassa ageukia madini.

  Iwapo nitashinda na kuwa rais, nitahakikisha mikataba mibovu ya madini na gesi inapitiwa tena ili kulinufaisha taifa...

Mgombea urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Edward Lowassa.
Mgombea urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Edward Lowassa, amesema iwapo atachaguliwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Uchaguzi Mkuu Oktoba 25 atahakikisha mikataba yote mibovu ya madini inapitiwa upya ili kujenga uchumi imara kwa manufaa ya taifa.
 
Lowassa ambaye alishaahidi kuifumua pia mikataba ya mafuta na gesi wakati akiwa mkoani Mtwara, aliyasema hayo jana kwenye mwendelezo wa mikutano yake ya kampeni katika kata ya Katoro, Jimbo la Busanda mkoani Geita.
“Iwapo nitashinda na kuwa rais, nitahakikisha mikataba mibovu ya madini na gesi inapitiwa tena ili kulinufaisha taifa,” alisema na kushangiliwa na maelfu ya watu waliojitokeza kwenye mkutano huo.
 
Mgombea huyo anayeungwa mkono pia na vyama vingine vinavyounda muungano wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), alisema mbali na kupitia mikataba ya madini na gesi, pia atahakikisha kuwa anaibadili Tanzania na kulikabili kwa ukamilifu tatizo la umaskini linalowakabili mamilioni ya wananchi. Kadhalika, alisema serikali atakayoiongoza itaboresha elimu na kilimo, ikiwa ni njia mojawapo ya kuwakwamua Watanzania kutoka kwenye lindi la umaskini.
 
SUMAYE, MGEJA 
Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye (pichani), alisema kuwa baadhi ya makada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wanawadanganya watu mchana kweupe kwa kuwaambia kuwa wakichagua wapinzani kutakuwa na vita kwani hakuna jambo hilo.“Mataifa yanayopigana vita ni yale ambayo viongozi wake wameng’ang’ania madarakani na wala siyo vinginevyo,”alisema.
 
Aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga, Khamis Mgeja, aliwataka wananchi wa Geita kumchagua Lowassa ili aondoe tatizo la uhaba wa ajira kwa vijana.
 
“Tanzania inahitaji kiongozi mwenye maamuzi magumu na muwajibikaji... huyu ni Lowassa peke yake. Hakikisheni hamdanganyiki na propaganda,” alisema Mgeja.
 
Katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 25, Lowassa ambaye ni Waziri Mkuu wa zamani, anatarajiwa kuchuana vikali na mgombea wa CCM, John Magufuli. Wagombea wengine ni Anna Mghwira wa ACT-Wazalendo, Janken Kasambala wa NRA, Fahmy Dovutwa wa UPDP, Maximillian Lymo wa TLP, Chifu Lutasola Yemba wa ADC na Hashim Rungwe wa Chaumma.
 
CHANZO: NIPASHE

2 comments :

  1. Her much information visit here to add insight to me then give useful for everyone. a visit back in jual jaket kulit asli... thank you

    ReplyDelete
  2. The first thing to visit this blog is useful information and provide comfort for visitors. a visit back in jaket kulit asli.... thank you

    ReplyDelete