Matokeo kwenye vituo yaonyesha walivyovuna kura, baadhi kupiga kura leo, mabomu ya machozi yarindima Dar, Mbeya, Mwanza na Moshi. Zanzibar nako hakijaeleweka...
Baadhi ya maeneo polisi walitumia mabomu ya kutoa machozi kuwatawanya wafuasi wa vyama vya siasa.
Mathalan, katika mikoa ya Dar es Salaam, Mwanza, Kilimanjaro, Mara na Mbeya, mabomu hayo yalirindima na kuwatawanya wafuasi wa vyama vya siasa waliokuwa na shauku kubwa ya kupata matokeo ya urais, ubunge na udiwani yatangazwe mapema.
Jijini Mwanza, mabomu yalianza kurindima katika kata ya Kitangiri saa 12:30 jioni wakijaribu kuwatawanya vijana waliokuwa wakisubiri matokeo na yaliendelea hadi saa 4:40 usiku katika maeneo hayo.
Hata hivyo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Charles Mkumbo, hakupatikana kuzungumzia hali hiyo.Katika mkoa wa Mara, mabomu ya machozi yalipigwa kusambaratisha makundi ya vijana waliokuwa wakitaka kutangaziwa haraka matokeo ya uchaguzi katika vituo kadhaa.
MATOKEO YA AWALI KWA BAADHI YA VITUO NI KAMA IFUATAVYO:-
KITUO CHA AMANA WEO ILALA
RAIS:
ACT 2, CCM 147, Chadema 144, Chaumma 0
NRA 0, TLP 0 UPDP 0 na zilizoharibika 5.
UBUNGE:
ACT 2, ADC 2, AFP 0, CCM 154, Chadema 113, CUF13, DP 0
Jahazi 0, TLP 0, UMD 0, kura zilizoharibika 11.
UDIWANI:
CCM 150, Chadema111, CUF 25, zilizoharibika 8.
Kituo cha Kiponza B1 Jimbo la Mbagala:
URAIS:
Chaumma 1, ACT 1, Chadema, 124, CCM 120 na zilizoharibika tatu
UBUNGE:
ACT 2, AFP 1, CCM 122, Chausta 3, CUF 111, DP 1, Jahazi 4, NCCR 2 na zilizoharibika 3.
UDIWANI:
ACT 9, AFP 2, CCM 115, Chadema 72, CUF 47 na zizilizoharibika 3.
MOSHI VIJIJINI:
Kituo cha Kimochi, Kisaseni:
URAIS:
CCM 49, Chadema 184
UBUNGE:
CCM 48, Chadema 185,
Diwani:
CCM 68, Chadema 165
Kituo cha Msasani - 1
URAIS:
CCM 60, Chadema 218
UBUNGE:
CCM 233, Chadema 44
URU MASHARIKI:
URAIS:
CCM 90, Chadema 175
UBUNGE:
CCM 91, Chadema 172
UDIWANI:
CCM 85, Chadema 182
Old Moshi Magharibi:
URAIS:
CCM 24, Chadema 203
UBUNGE:
CCM 29, Chadema 198
MANDAKA MNONO A
URAIS CCM 72, Chadema 87
UBUNGE:
CCM 72, Chadema 87
WERUWERU 2
URAIS:
CCM 67, Chadema 163
UBUNGE:
CCM 88, Chadema 182
KINDI JUU (3)
URAIS:
CCM 78, Chadema 197
UBUNGE:
CCM 84, Chadema 189
Kata ya Azimio, kituo cha Shule ya Msingi mji Mpya A2; Edward Lowassa 130, Dk. John Magufuli 75, Hashimu Rungwe 2, Anna Mghwira 0, Chief Lutasola Yemba 0, Fahmi Dovutwa 0, Maxmillian Lyimo 0.
Kituo cha Kigamboni 3: Anna Mghwira 1, Chifu Lutasola Yemba, Dk. Magufuli 120, Edward Lowassa 136, Hashim Rungwe 1, Janken Kasambala 0, Maximillian Lyimo 0 na Fahmi Dovutwa 0.
UBUNGE
Diana Joseph (ACT) 3, Lea David (TLP) 0, Dk Ndugulile (CCM) 131, Lucy Magirili (Chadema) 109, Rungwe Chama 2 na Juma Nkumbi 8.
UDIWANI
Dotto Msawa (CCM) 139, Mustafa Kiasi (CUF) 116
JIMBO LA TEMEKE
KITUO CHA SHULE YA SEKONDARI MBANDE
URAIS
CCM 427, Chadema 579, Chauma 2, UPDP 1, ACT 1.
UBUNGE
UDP 2, NCCR-Mageuzi 8, AFP 7, ACT 23, Chausta 8,NRA 3, Tadea 4, CUF 510, CCM 233 na DP 1, Jahazi 4 na UPDP 1,Makini 1.
UDIWANI
ACT 20, Chausta 3, UDP 3, Chadema 292, CUF 274, CCM 405, UMD 1 na AFP 2.
JIMBO LA ARUSHA MJINI
KITUO CHA KALOLENI SEKONDARI Na.1
UDIWANI
CCM 149. Chadema 133, Urais cdm 166. Ccm 120
KALOLENI Na. 2
UDIWANI
Chadem 122, CCM 158,
URAIS
Chadema 161. CCM 126.
Kaloleni sekondari Na. 4, Udiwani, CCM 168, Chadema 107, Urais CCM 138, Chadema 141.
Kituo cha AICCc nursery Na. 1. Udiwani CCM 98, Chadema 250, Urais Chadema 269, CCM 81
Kituo AICC nursery Na. 5, Urais Chadema 248, CCM 111, Udiwani Chadema 241, CCM 109.
Kituo cha Ofisi ya Afisa Mtendaji kata ya Mtoni.
URAIS
Lowassa 134, Magufuli 113, Hashimu Rungwe 1, vyama vingine zero.
UBUNGE
CCM 117, CUF 108, UPDP 2, TLP 1, CHAUMA 5, AFP 1 na ACT-Wazalendo 7.
ARUMERU MAGHARIBI
Jimbo la Arumeru Magharibi, katika Kata ya Kiutu, kituo cha shule ya msingi Naurei 1 Rais Chadema 276, CCM 47, ACT 01 na TLP 0.
Kwa upande wa ubunge Ubunge CCM 43, CHADEMA 270 , ACT 3. Kwa udiwani CCM35, CHADEMA 249 na ACT 6.
Kata ya Kiutu kituo cha pili Jimbo Arumeru Magharibi
URAIS
ACT-Wazalend0 – 1, Chadema – 254, CCM – 55
UDIWANI
CCM – 48, Chadema -227, ACT – Wazalendo - 3
UBUNGE
CCM – 47, Chadema – 258, ACT – Wazalendo - 3
DODOMA
Katika Manispaa ya Dodoma kituo cha Shule ya Msingi Uhuru namba 3 Kata ya Uhuru kwa udiwani CCM 97, CHADEMA 92. Ubunge CCM 101 na CHADEMA 86 w. Urais CCM 108 na Chadema 81.
Kituo cha Weo namba 1 katika Kata ya Viwandani, urais CCM 131, CHADEMA 92. Ubunge CCM 130 na Chadema 89.
Kituo cha Weo namba 2, urais CCM 126, CHADEMA 80 wakati ubunge CCM 122 na CHADEMA 77.
Kituo cha Moku Security Guard namba 1, urais CCM 127 na CHADEMA 140. Ubunge, CCM 125 wakati Chadema ni 139.
Kituo cha Moku Security Guard namba 2., urais CCM 143, CHADEMA 85. Ubunge CCM 135 , Chadema 89.
Kituo cha ofisi ya mwenyekiti mtaa wa Baruti namba 2, urais CCM 160, CHADEMA 101. ubunge CCM 151,
CHADEMA 107.
Kituo cha Samora namba 1, urais CCM 125, CHADEMA 91. Ubunge CCM 121, CHADEMA 90.
Kituo cha NHC, urais CCM 144, CHADEMA 138. Ubunge CCM 137, Chadema 141.
MOSHI VIJIJINI
Kituo cha Kimochi, Kisaseni. Urais CCM 49, Chadema 184. Ubunge CCM 48, CHADENA 185. Udiwani CCM 68, CHADEMA 165.
Kituo S/M MSASANI-1, urais CCM 60, CHADEMA 218. Ubunge CCM 233, CHADEMA 44
Kituo cha URU Mashariki urais CCM 90, CHADEMA 175. Ubunge CCM 91, CHADEMA 172. Udiwani CCM 85, CHADEMA 182.
Kituo cha Old Moshi Magharibi. Urais CCM 24, CHADEMA 203. Ubunge CCM 29, CHADEMA 198.
Kituo Mandaka Mnono A. Urauis CCM 72, CHADEMA 87.
Kituo cha Weruweru 2, urais CCM 67, CHADEMA 163. Ubunge CCM 88, CHADEMA 182.
JIMBO LA KAWE
Kituo Jangwani Beach B 3
URAIS
CCM- 124, Chadema- 127, ACT-Wazalendo -2 na ADC-2.
UBUNGE
CCM-107, Chadema- 137, ACT-Wazalendo- 6, ADC- 1, Tadea 1
UDIWANI
CCM-119, Chadema-126, ACT - 4, CUF-1
Kituo cha Jangwani B2
Urais
ACT-Wazalendo-0, CCM- 82, Chadema-125, Chauma 0.
Ubunge
ACT-Wazalendo-4, CCM-79, Chauma- 2, CUF-116, AFP- 0, Chausta-1, DP- 0, TLP 0,UPDP-2.
Udiwani
ACT-Wazalendo- 2, CCM-79, Chadema-46, Chaumma 0, Cuf- 77.
Urais
ACT-Wazalendo- 2, CCM- 140, Chadema -127, Chauma -1, NRD-0.
Ubunge
ACT-7, CCM- 127, Cuf- 128, Chauma- 4, AFP-1,Chausta- 0, TLP-2.
Urais
CCM-98, Chadema -135,
Ubunge
ACT-4, ADC-1, CCM-89, Cuf- 128, DP- 0, TLP-2, UPDP- 0, Chausta- 2.
Udiwani
ACT-3, CCM- 86, Chadema -50, Cuf- 90.
JIMBO LA UBUNGO
Kituo kupigia kura shule ya Mugabe.
CCM- 104, Chadema- 131,
Kituo Dar Inter School A1,
CCM 104, Chadema 149, ACT 01,
Kituo DSM inter trust sec school,
CCM 130, Chadema 198,TLP 02,
Kituo shule us msingi Mugabe,
CCM ,124, Chadema 145, Chaumwa 01,
Kituo cha Mugabe A3,
CCM 128, Chadema 118,
Kituo cha Mugabe 04,
CCM 119, Chadema 168
Mtwara
Kituo cha Technical- 2,
URAIS
ACT – Wazalendo - 1, ADC – 0, CCM – 53, Chadema – 73, Chaumma – 0, NRA – 0, TLP – 0, UPDP – 0
UBUNGE
ACT – 2, CCM – 55, Chadema – 30, Cuf -40, NCCR-Mageuzi -0
UDIWANI
CCM – 58, Chadema – 63, Cuf - 5
Kituo B Shule ya Winning Spirit
URAIS
CCM- 80, Chadema -271, ACT – 0
UBUNGE
CCM - 66, Chadema - 278, ACT- Wazalendo 3, udiwani CCM 64, Chadema 278, ACT- Wazalendo - 3
Kituo cha Win Spirit B –1
URAIS
CCM - 64, Chadema – 289, ACT-Wazalendo – 1, Chaumma - 2
UBUNGE
CCM -49, Chadema – 303, ACT-Wazalendo – 2
UDIWANI
CCM – 51, Chadema -298, ACT- Wazalendo - 7
Shule ya Msingi Charambe
URAIS
ACT – Wazalendo – 2, CCM – 118, Chadema 133
UBUNGE
ACT-Wazalendo – 7, ADC- 2, AFP – 1,
CCM – 124, Demkrasia Makini – 1, NCCR – Mageuzi – 3, Cuf 111, Jahazi Asilia – 1, Chausta - 1
UDIWANI
ACT – Wazalendo – 5, CCM – 118, Chadema – 63, Cuf - 65
Matokeo kituo cha Sharif Shamba Ilala
URAIS
ACT – Wazalendo – 0, ADC – 0, CCM – 130, Chadema – 172, Chadema – 2, NRA – 0, TLP – 0, UPDP - 0
UBUNGE
ACT- Wazalendo – 4, ADC – 0,
AFP – 0, CCM – 148, Chadema – 139, Cuf -6, DP – 0, Jahazi Asilia – 0, UPDP - 0
UDIWANI;
CCM – 130, Chadema – 153,
Cuf - 12
Kituo cha Charambe Shule A-2
URAIS
CCM – 108, Chadema -137
UBUNGE
ACT -7, ADC – 1, CCM – 114, Chausta – 3,
Cuf – 115, DP -1, NCCR - Mageuzi – 4, NRA - 2
UDIWANI
ACT 5, CCM – 102, Chadema -71, Cuf - 68
Mlimani Sekondari- 1 kata ya Pamba Jimbo la Nyamagana
URAIS
CCM – 130, Chadema – 137, ACT – Wazalendo - 1
UBUNGE
CCM- 108, Chadema – 151, ACT – Wazalendo 1, Cuf - 1
Kituo cha Mlimani Sekondari -2
URAIS
CCM – 129, Chadema -116, ACT-Wazalendo 1
UBUNGE
CCM - 111, Chadema – 131, NRA – 1, ACT - Wazalendo 3
Kituo cha Shule ya Msingi Mlimani - 1
URAIS
CCM – 141, Chadema – 121, ACT- Wazalendo - 1
UBUNGE
CCM – 117, Chadema 139, ACT – Wazalendo - 1
Kituo cha Shule ya Msingi Mlimani- 2
URAIS
CCM – 137, Chadema – 89, Chaumma -2, ACT – Wazalendo 1, ADC -1
UBUNGE
CCM – 117, Chadema -109, ACT-Wazalendo – 1, Jahazi Asilia - 1
Kituo cha Mlimani B-1
URAIS
Chadema -137, CCM 109, ACT – Wazalendo 3, ADC - 1
UBUNGE
CCM- 72, Chadema – 154, ACT – Wazalendo 2
Kituo cha Mlimani B- 2
URAIS
CCM – 139, Chadema - 121
UBUNGE
CCM 109, Chadema – 144, Cuf – 27, ACT-Wazalendo 3, Jahazi Asilia - 1
Kituo cha Mlimani C -1
URAIS
CCM – 115, Chadema – 123, ACT- Wazalendo – 2
UBUNGE
CCM 84, Chadema – 155,
Kituo cha Mlimani C - 2
URAIS
Chadema – 138, CCM- 115,
Chaumma -1
UBUNGE
CCM – 86, Chadema – 158, Cuf – 1, ACT-Wazalendo - 1
Kituo cha Mlimani A- 1
URAIS
Chadema -148, CCM - 130
UBUNGE
Chadema – 166, CCM 111, ACT- Wazalendo - 2
Kituo cha Mlimani A- 2
URAIS
CCM- 162, Chadema – 133, ADC – 1, ACT- Wazalendo - 1
UBUNGE
CCM – 139, Chadema – 156, ACT – Wazalendo 2, Cuf - 2
Kituo Kata ya Mbugani C- 2
URAIS
CCM – 168, Chadema - 124
UBUNGE
CCM- 145, Chadema - 144
Kituo Kata ya Mbugani C- 1
URAIS
CCM -162, Chadema – 130, ACT- Wazalendo - 1
UBUNGE
CCM- 135, Chadema- 154, ACT-Wazalendo – 1
Kituo cha Mbugani B- 2
URAIS
CCM -145, Chadema -132, ACT – Wazalendo – 1, TLP - 1
UBUNGE
CCM – 125, Chadema – 148, Cuf – 3, ACT-Wazalendo - 2, UDP - 2
Kituo cha Mbugani B - 1
URAIS
CCM – 139, Chadema – 142, Chaumma - 2
UBUNGE
CCM – 110, Chadema – 169, ACT- Wazalendo – 1, Cuf -1
Kituo cha Mbugani A - 1
URAIS
CCM – 107, Chadema – 107, ACT- Wazalendo - 1
UBUNGE
CCM – 86, Chadema – 117, ACT- Wazalendo – 3, Cuf -4
Kituo cha Mbugani A - 2
URAIS
CCM 121, Chadema – 94, ACT-Wazalendo – 1, Chaumma - 1
UBUNGE
CCM – 124, Chadema- 102, ACT-Wazalendo -4
Kituo cha Mbugani B - 3
URAIS
CCM – 155, Chadema- 133
UBUNGE
CCM 132, Chadema – 140, ACT-Wazalendo – 3, Cuf - 1
Awali, mamilioni ya Watanzania, vijana, wanawake na hata wazee, jana waliamka alfajiri kwenda katika vituo vya kupigia kura kuamua viongozi wao watakaowaongoza katika kipindi cha miaka mitano ijayo huku utulivu ukitawala katika maeneo mengi nchini.
Wapigakura walionekana vituoni wakiwa kwenye misururu mirefu, pasipo kuwapo vurugu kati yao ama dhidi ya walinzi wa usalama hasa askari polisi waliokuwa wanafanya doria.
Barabara za Jiji la Dar es Salaam na miji mingi ya nchi ikiwamo Mwanza, Arusha, Zanzibar na Mbeya, zilikuwa na magari machache huku usafiri wa umma ukiwa wa taabu.
Maeneo ya biashara kama maduka, migahawa na nyumba nyingi za ibada, vilifungwa kutokana na muitikio wa watu kushiriki Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu.
Wanawake wenye watoto wadogo, vijana na vikongwe, walionekana kwa wingi vituoni, ikiwa ni tofauti na chaguzi zilizopita, ilipoaminika kwamba ni wachache tu walioshiriki kupiga kura.
Hata hivyo, licha ya mafanikio hayo, bado uchaguzi huo ulikabiliwa na kasoro kadha wa kadha Tanzania bara sambamba na Tanzania Visiwani ikiwamo kuchelewa kwa vifaa, wasimamizi, kufunguliwa kwa vituo vya kupigia kura na watu wengi kutoyaona majina yao kwenye orodha ya wapigakura.
Wagombea waliopigiwa kura jana ni wanaowania nafasi za Rais wa Muungano, Rais wa Zanzibar, wabunge, wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar nam madiwani.
Hata hivyo, ushindani mkubwa katika uchaguzi huo ni katika ‘kurithi’ kiti cha urais kinachoachwa na Rais Jakaya Kikwete anayemaliza miaka 10 ya utawala wake.
Ushindani huo ukawa kati ya mgombea kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. John Magufuli na Edward Lowassa, wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) aliyeungwa mkono na vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).
Wagombea wengine walikuwa ni Anna Mghwira (ACT- Wazalendo), Janken Kasambala (NRA), Fahmi Dovutwa (UPDP), Chifu Lutasola Yemba (ADC) na Hashim Rungwe (Chaumma).
Hata hivyo, ni Magufuli na Lowassa waliowaaminisha wafuasi wao na umma kuwa na uhakika wa kushinda.
Lakini walipohojiwa jana kwa nyakati na mahali tofauti, Magufuli na Lowassa walijielekeza katika kuzungumzia mwenendo wa uchaguzi huo huku wakikwepa kutumia kauli zenye majigambo ya ushindi.
MAGUFULI APIGA KURA CHATO
Magufuli alipiga kura katika kituo cha Shule ya Msingi Magufuli iliyopo katika kijiji cha Rubambangwe, kata ya Muungano wilayani Chato. Aliwasili kituoni saa 4:30 asubuhi akitokea Mwanza alikohitimisha kampeni zake juzi.
Baada ya kumaliza kupiga kura, Magufuli hakuzungumzia hali ilivyokuwa wakati wa kampeni na kusema atafanya hivyo ikiwa atashinda na kuapishwa kuwa Rais wa awamu ya tano.
Akizungumzia hali ilivyokuwa jimboni hapo, Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo la Chato, Joel Hari, alisema hakuna dosari kubwa zilizoripotiwa kutoka kwenye vituo vya kupigia kura na kwamba, wanatarajia kukamilisha mchakato huo kwa amani na utulivu.
Baadhi ya wakazi wa Chato walieleza kuwa wamefurahishwa na utaratibu uliowekwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec) kupanga majina kwa kufuata mtiririko wa herufi ili kurahisisha kuonekana kwa ufasaha na haraka.
LOWASSA ARIDHISHWA MONDULI
Lowassa alipiga kura katika kituo cha Ngarash, kata ya Engutoto, wilayani Monduli, huku akisema ameridhishwa na jinsi upigaji kura ulivyokuwa ukiendelea.
Lowassa alisema kwa ujumla, upigaji kura alioushuhudia kituoni hapo alipopiga kura saa 3:00 asubuhi ulifanyika kwa amani na utulivu.
Lowassa alisema atakubali matokeo ikiwa kazi ya upigaji kura itaendelea kuwa huru na haki pasipokuwa na dosari.
“Nitakubali matokeo ya ushindi, nitakubali pia matokeo iwapo nitashindwa kama tu zoezi hili litaendelea kuwa huru na haki pasipo mizengwe,” alisema Lowassa wakati akizungumzaa na waandishi wa habari baada ya kupiga kura. Kuhusu tuhuma za baadhi ya watu kukakamatwa wakiwa na kura zilizopigwa, alisema watu hao wanapaswa kushtakiwa na kufungwa.
Hata hivyo, aliiomba Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec) kuongeza umakini zaidi katika kusimamia uchaguzi hadi kufikia hatua ya mwisho ya kutangaza matokeo.
UTULIVU ARUSHA
Upigaji kura kwenye maeneo mengi jijini Arusha umefanyika kwa amani licha ya watu wengi kulalamika hawakuyaona majina yao kwenye orodha ya wapiga kura.
Tukio hilo lilijitokeza zaidi katika kituo cha Ebeneza, kata ya Murriet. Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Msasasi kilipo kituo hicho, Joshua Mwanga alisema majina ya wapigakura 544 hayakuwamo kwenye orodha hiyo.
Hata hivyo, alisema baada ya kuwasiliana na afisa mtendaji wa kata hiyo, walishughulikia suala hilo na watu 150 kati ya hao walipiga kura.
CHANZO: NIPASHE
No comments :
Post a Comment