Baada ya tambo zilizodumu kwa siku 90 za kampeni za Uchaguzi Mkuu, Watanzania wanafanya maamuzi magumu leo.
Wanapiga kura ya kuwachagua marais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Zanzibar, wabunge, wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar na madiwani.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec), Jaji Damian Lubuva, Watanzania 23,782,558 wanatarajiwa kupiga kura kwenye vituo 37, 848 (vinavyoweza kuongezwa) na ambavyo vitafunguliwa kuanzia saa 2:00 asubuhi hadi saa 12:00 jioni.
Wapigakura katika kituo kimoja watapiga kura ndani ya dakika 540 ambazo ni sawa na dakika 1.2 kwa kila mtu.
Wachambuzi wa masuala ya siasa wanasema tofauti na uhalisia kutokana na Nec kupitia Sheria ya Uchaguzi kufafanua watu watakaokuwa katika mistari mpaka saa 12:00 wataendelea kupiga kura mpaka watakapomalizika.
KAMPENI ZA USHINDANI
Ni kampeni zilizokuwa na ushindani mkubwa unaosadikiwa kutoonekana nchini tangu kuanza kwa mfumo wa vyama vingi mwaka 1992.
Ushindani huo ukakolezwa zaidi na hatua ya viongozi kadhaa waliokuwa katika ngazi za taifa, mkoa na wilaya katika Chama Cha Mapinduzi (CCM) na serikali yake, walioongozwa na Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa kujiunga upinzani.
MAGUFULI NA LOWASSAWanapiga kura ya kuwachagua marais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Zanzibar, wabunge, wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar na madiwani.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec), Jaji Damian Lubuva, Watanzania 23,782,558 wanatarajiwa kupiga kura kwenye vituo 37, 848 (vinavyoweza kuongezwa) na ambavyo vitafunguliwa kuanzia saa 2:00 asubuhi hadi saa 12:00 jioni.
Wapigakura katika kituo kimoja watapiga kura ndani ya dakika 540 ambazo ni sawa na dakika 1.2 kwa kila mtu.
Wachambuzi wa masuala ya siasa wanasema tofauti na uhalisia kutokana na Nec kupitia Sheria ya Uchaguzi kufafanua watu watakaokuwa katika mistari mpaka saa 12:00 wataendelea kupiga kura mpaka watakapomalizika.
KAMPENI ZA USHINDANI
Ni kampeni zilizokuwa na ushindani mkubwa unaosadikiwa kutoonekana nchini tangu kuanza kwa mfumo wa vyama vingi mwaka 1992.
Ushindani huo ukakolezwa zaidi na hatua ya viongozi kadhaa waliokuwa katika ngazi za taifa, mkoa na wilaya katika Chama Cha Mapinduzi (CCM) na serikali yake, walioongozwa na Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa kujiunga upinzani.
Magufuli aliianza safari ya kuwania urais akitokea CCM alipoelezwa kutokuwa na makundi kama ilivyokuwa kwa baadhi ya wagombea.
Akionekana kudhamiria ‘kuibeba’ zaidi CCM, Magufuli hakujinadi kwa ahadi binafsi namna atakavyoingoza nchi ikiwa atateuliwa na chama hicho kuwania na kushinda kiti cha urais.
Alipokuwa katika kutafuta udhamini ndani ya CCM, Dk. Magufuli alisisitiza kuwa ahadi zake zitatokana na ilani ya uchaguzi ya chama hicho, hali iliyomfanya aanze kuaminika kuwa anastahili kuwania nafasi hiyo.
Licha ya kutokuwa na makundi, Magufuli akajijengea heshima ya kutokuwa na kashfa zitakazomfanya atumie muda mwingi kujisafisha. Lakini rekodi ya utendaji kazi wake nayo ikawa miongoni mwa ‘nyenzo’ zilizomfikisha katika kampeni za uchaguzi wa leo kwa imani ya ushindi.
Wakati Magufuli akiteuliwa na CCM kuwania urais, Edward Lowassa aliyekuwa anawania fursa hiyo kupitia chama hicho ‘akakatwa’, hivyo kuamia kujiunga katika Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).
Lowassa aliaminika kuwa na nafasi kubwa ya kuteuliwa na CCM kutokana na kuwa na watu wengi waliomuunga mkono ndani na nje ya CCM, lakini ‘kukatwa’ kwa jina lake kukamuondoa kwenye chama alichokitumikia kwa takribani miongo miwili.
Julai 27, mwaka huu Lowassa alikaribishwa kujiunga na vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).
Julai 28, mwaka huu, Lowassa alijiondoa CCM na kujiunga rasmi katika Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) alipochukua fomu za kuwania urais kupitia chama hicho, Julai 31 na kuzirejesha Agosti Mosi, mwaka huu.
Kuingia kwa Lowassa katika Chadema kulisababisha viongozi akiwamo Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye wanachama na wafuasi wengi wa CCM kujiunga upinzani.
Hatua hiyo ilichagiza ushindani mkubwa wa kisiasa katika kampeni za uchaguzi huo kati ya yake (Lowassa) na Magufuli. Ingawa hatumii muda mwingi kuhutubia, Lowassa ‘anaogopwa’ kwa namna anavyomudu kupanga na kutekeleza mikakati ya uchaguzi.
Mbali na Magufuli na Lowassa, wagombea urais wengine waliofika kwenye eneo kubwa la nchi na kusikilizwa na wapiga kura ni Mghwira na Rungwe.
Pia walikuwapo wagombea urais wengine Machmillan Lyimo (TLP), Chifu Lutalosa Yembe (ADC), Fahmi Dovutwa (UPDP), Hashim Rungwe (Chauma), Anna Mghwira (ACT Wazalendo) na Janken Kasambala (NRA).
Ushindani uliokuwapo katika kampeni hizo ulichangia wagombea katika ngazi tofauti kuwafikia wananchi kwa karibu, wakiwashawishi wawachague katika uchaguzi wa leo.
Wagombea waliwafikia wapigakura kupitia ziara za mtaa kwa mtaa, mikutano ya hadhara, vyombo vya habari na kubandika mabango yenye picha zao na bendera za vyama vilivyowateua.
Mitaa ya mijini na maeneo ya vijijini yaliwekwa mabango na bendera hizo, hivyo kuchagiza kasi ya ushindani unaofanya uchaguzi wa leo kufuatiliwa kwa karibu.
MBINU ZA KAMPENI
Kutokana na ushindani huo, wagombea wa nafasi mbalimbali walitumia mbinu tofauti kujinadi kwa wapigakura.
Kwa upande wake, upinzani ulijikita zaidi katika kuikosoa serikali ya CCM na namna ilivyoshindwa kufikia malengo ya utekelezaji wa ahadi zilizotolewa katika Uchaguzi Mkuu wa 2010.
Pia wapinzani walitumia mianya iliyopo katika changamoto kama huduma duni za kijamii, ubovu wa miundombinu na uwezo mdogo wa nchi katika kukabiliana na magonjwa.
Hoja nyingine za upinzani zilielekezwa katika matumizi mabaya ya rasilimali za umma na aina nyingine zilizokwamisha jitihada za kukuza uchumi na kustawisha maisha ya watu.
Kwa hali hiyo, mgombea urais kupitia Chadema inayoungwa mkono na Ukawa, Lowassa akajipambanua kuzimudu changamoto hizo kwa kuwekeza zaidi katika uboreshaji wa elimu na kwamba serikali yake (akichaguliwa) itagharamia elimu kuanzia ya awali hadi Chuo Kikuu.
Hata hivyo hoja kama hiyo ikajitokeza kwa CCM na ACT Wazalendo walioelezea katika ilani zao cha uchaguzi kwamba uboreshaji wa sekta hiyo utafanyika kwa kutoa elimu bure, ingawa kwa CCM ikaeleza kutoa elimu bure hadi kiwango cha sekondari.
UAMUZI MGUMU
Kwa namna kampeni za mwaka huu zilivyofanyika na muitikio wa watu wakiwamo wanaotoka nje ya nchi, ni dhahiri kwamba kesho utafanyika uamuzi ulio mfano wa hukumu yenye kuelezea anayestahili kuongoza kwa miaka mitano ijayo.
Tofauti na chaguzi zilizopita ambapo CCM ilijihakikishia ushindi hata kabla ya kura kupigwa, matokeo ya uchaguzi wa leo yatasubiriwa hadi dakika ya mwisho kura zitakapohesabiwa na jumla yake kutanganzwa na mamlaka husika.
Kwa mujibu wa sheria za uchaguzi nchini, matokeo ya wagombea ubunge na udiwani yanatangazwa na Mkurugenzi Mtendaji (DED) wakati ya urais yanajumuishwa na kutangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec).
MGHWIRA ASHANGAZA
Katika hali ambayo haikutarajiwa, mbombea urais kupitia ACT Wazalendo, Mghwira akafika eneo kubwa la nchi akijinadi kwa namna atakavyoiongoza Tanzania ikiwa atachaguliwa katika uchaguzi wa leo.
Akiwa mwanamke pekee anayewania urais katika uchaguzi huo, akitokea `chama kichanga’ kilichopata usajili wake Mei 5, mwaka jana, Mghwira akazimudu kampeni kuliko wagombea wa vyama ‘vikongwe’ katika siasa za mageuzi.
Ingawa kuna uwezekano wa wagombea urais kupitia vyama kama TLP, NRA na UPDP kwenda kwenye mikoa kadhaa, lakini wananchi walipata fursa ya kumsikiliza zaidi Mghwira ikiwamo kupitia vyombo vya habari.
RUNGWE AWAVUTIA VIJANA
Mgombea kupitia Chama cha Umma (Chaumma), Hashim Rungwe, alionekana akifanya mikutano ya kampeni kwenye maeneo yenye mikusanyiko ya watu, hivyo kuwavutia watu wengi hasa vijana.
Akionekana kutokuwa na ilani ya uchaguzi iliyomuongoza na kuitumia kwenye mikutano kadhaa, Rungwe aliwasilisha ushawishi wake kwa kutumia maneno yanayoeleweka kwa urahisi hasa na vijana.
Hali hiyo ilimfanya, licha ya kutokuwa na vivutio kama vyombo vikubwa vya muziki ama wasanii wa fani tofauti, mikutano yake ilihudhuriwa na watu waliomsikiliza kwa namna inayoweza kumfanya akapata kura katika uchaguzi wa leo.
WAGOMBEA WENGINE KIMYA KIMYA
Wagombea wengine wakiwamo wa urais kupitia vyama kama TLP, ADC, UPDP na NRA hawakuonekana sana katika kampeni, hali iliyozua hisia kuwa huenda walikuwa na mbinu za kupita mtaa kwa mtaa ama hawakushiriki kabisa.
Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi anasema hali hiyo inaweza kutazamwa na wadau wa uchaguzi, ingawa itakuwa vigumu kupata suluhu linalolenga kuwabana wasishiriki chaguzi nyingine.
Jaji Mutungi anasema kushiriki uchaguzi kunategemea mbinu na matumizi ya rasilimali kwa kadri chama ama mgombea alivyojipanga, ili mradi asivunje Sheria ya Gharama za Uchaguzi.
“Inawezekana wanashiriki kampeni kwa mbinu zao zilizo tofauti na hizi za hawa tunaowaona kwenye majukwaa kila siku,” anasema Jaji Mutungi.
CHANZO: NIPASHE JUMAPILI
No comments :
Post a Comment