Kamanda wa Polisi mkoa wa Tanga Zuberi Mwombeji
Tanga. Msimamizi wa Uchaguzi kata ya Pagwi wilayani Kilindi Rajabu Nkungua amefariki dunia baada ya gari alilokuwa akitumia kusafirisha kura kutoka ngazi kwenda halmashauri kupinduka.
Ajali hiyo imetoka jana majira ya saa 1.30 asubuhi huko wilayani Kilindi amabpo gari alilokuwa akitumia Mtendaji Kata huyo kupasuka tairi ya mbele na kupinduka.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Tanga Zuberi Mwombeji alithibitisha kutokea kwa kifo hicho na kusema kuwa masanduku kura yakifanikiwa kutolewa salama.
Alisema Polisi inaendelea na uchunguzi wa tukio hilo ili kujua chanzo halisi cha ajali hiyo.
Wakati huo huo Jeshi la Polisi mkoani Tanga linawashikilia watu nane na linamsaka aliyekuwa mgombea wa Kata ya Kisiwani Gideon Sebarua katika Jimbo la Bumbuli wilayani Lushoto kwa tuhuma za kufanya uharibifu wa masanduku ya kura.
Akizungumzia mazingira ya tukio hilo Kamanda wa Polisi mkoa wa Tanga Zuberi Mwombeji alisema watuhumiwa hao walifanya vurugu wakati masanduku ya kura yakipelekwa kwenye ngazi ya Jimbo.
Kamanda Mbombeji alisema tukio hilo lilitokea majira ya saa 7.00 usiku katika Kata ya Kisiwani,Jimbo la Bumbuli wilayani Lushoto.
"Wakati wakiwa wanapeleka masanduku ya kura kwa msimamizi wa Jimbo ndipo vurugu zilipojitokeza na kusababisha uharibifu wa baadhi ya mali hasa kwa baadhi ya masanduku hivyo tunamsaka mgombea huyo ili sheria ichukue mkondo wake",alisema Kamanda huyo.
No comments :
Post a Comment