dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Tuesday, October 20, 2015

Tumewandaa vipi Watanzania kupokea matokeo?

Mlemavu asiyeoona akisoma mfano wa karatasi ya Kupigia Kura wakati wa Mkutano kati ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC, Picha na Tume ya Uchaguzi
By Daniel Mjema ,Mwananchi
Oktoba 25, Watanzania milioni 22 wanatarajia kupiga kura kumchagua rais, wabunge na madiwani, lakini swali kuu ni je, vyama vya siasa vimewaanda wanachama wao kisaikolojia kupokea matokeo?
Nauliza swali hilo kwa sababu mchuano baina ya mgombea urais wa Chadema, Edward Lowassa na wa CCM, Dk John Magufuli ni mkali na usiowahakikishia wagombea hao ushindi kwa asilimia 100.
Hata kama Dk Magufuli au Lowassa wataegemea umati wa watu waliohudhuria mikutano yao kama kigezo cha kuthibitisha kukubalika kwao, basi wagombea wote hao wawili walijaza viwanja kwa umati.
Lakini ukweli ni kwamba wingi wa watu mikutanoni si kigezo cha ushindi kwa sababu mtu anaweza kukuchekea usoni, lakini moyoni hayuko nawe.
Tatizo langu si kwa wagombea hawa kwani wote wanajua kuna kushinda au kushindwa kwa haki, lakini, wafuasi wameandaliwa vipi kuyapokea matokeo hayo, yawe mabaya au mazuri kwao?
Ndiyo maana nimetangulia kuuliza, wameandaliwa vipi kisaikolojia? Kama hatujawaandaa, ni wazi upande wowote unaweza kuamini umeshinda hata kama umeshindwa kihalali.
Bahati mbaya, Katiba, haitoi fursa kwa aliyeshindwa kuhoji matokeo hayo mahakamani. Ibara ya 41(7) ya katiba hiyo inasema endapo mshindi wa kiti cha rais ameshatangazwa na NEC, hakuna mahakama yoyote nchini itakayokuwa na mamlaka ya kuchunguza kuchaguliwa kwake.
Katika mazingira haya ambayo huwezi kuhoji, ni dhahiri vyama vya siasa vinapaswa kuwaandaa wafuasi wao kisaikolojia, kuamini kuwa matokeo yatakayotangazwa na NEC ni halali.
Nayasema haya nikiegemea yale yaliyotokea nchini Kenya mwaka 2007, baada ya nchi hiyo kuingia kwenye machafuko baada ya Mwai Kibaki kutangazwa kuwa mshindi katika uchaguzi huo.
Uchaguzi huo unafanana na huu wa kwetu, kwamba kulikuwa na ushindani mkubwa kati ya Kibaki na Raila Odinga, lakini mwishowe Tume ya Uchaguzi ya Kenya ikamtangaza Kibaki kuwa mshindi.
Kura ya maoni iliyoendeshwa nchini humo kama ilivyofanyika hapa nchini, ilimpa Odinga ushindi wa asilimia 50 akifuatiwa na Kibaki asilimia 39 na Kalonzo Musyoka asilimia nane.
Lakini kura nyingine ya maoni iliyofanyika Novemba, ikiwa ni mwezi mmoja tu kabla ya uchaguzi huo ikaonyesha Kibaki na Raila walikuwa wamefungana kwa kupata asilimia 43.6 na 43.3 ya kura. Kura zilipopigwa Desemba 27 Kibaki aliibuka na ushindi wa asilimia 47 na Odinga asilimia 44.
Kutokana na wafuasi kutoandaliwa kisaikolojia kupokea matokeo, nchi hiyo iliingia kwenye machafuko ambayo Wakenya zaidi ya 1,200 walipoteza maisha.
Hapa Tanzania, taasisi ya Twaweza iliyofanya utafiti ilionyesha kuwa kama uchaguzi ungefanyika Septemba, basi Dk Magufuli angepata asilimia 66 dhidi ya asilimia 22 za Edward Lowassa.
Matokeo hayo ya tafiti yalilalamikiwa na Umoja wa Katiba ya Katiba (Ukawa) kuwa yaliandaliwa kuibeba CCM na kwamba mgombea wao angeibuka na ushindi wa asilimia 76 za kura zote.
Ndiyo maana tangu mwanzo nilitangulia kuhoji tumewaandaje Watanzania kupokea matokeo? Tayari tumesikia baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa wakiwataka wafuasi wao kukaa mita 200 kutoka kituo cha kupigia kura ili kulinda kura. Tujiulize wanaandaliwa vipi kuyapokea matokeo?
Tukishaanza kuwaandaa wafuasi wetu kuwa tutaibiwa kura, badala ya kuwaandaa kupokea matokeo yawe mabaya au mazuri, tutalitumbukiza Taifa letu kwenye machafuko na sote tutakuwa waathirika.

No comments :

Post a Comment