Mwangalizi Mkuu wa ujumbe wa waangalizi wa Umoja wa Ulaya (EU), Judith Sargentini
Dar es Salaam. Mwangalizi Mkuu wa ujumbe wa waangalizi wa Umoja wa Ulaya (EU), Judith Sargentini anasema kumekuwa na hali ya utulivu katika vituo 400 vilivyotembelewa na waangalizi wa EU nchi nzima.
Anasema watu wamejitokeza kwa wingi na wanapiga kura katika hali ya utulivu na taratibu zinafuatwa licha ya kasoro ndogondogo zilizojitokeza kama vile kuchelewa kufunguliwa kwa vituo.
Mwangalizi huyo amewataka mawakala na wasimamizi wa Uchaguzi kutimiza wajibu wao katika kuhakikisha mshindi halali anapatikana.
"Kwa ujumla upigaji kura unaenda vizuri na watu wanaonekana kufuata taratibu. Bado sehemu ya pili muhimu ambayo ni kuhesabu kura. Ninawaomba mawakala na wasimamizi kila mmoja atimize wajibu wake," alisema.
Mwangalizi huyo anasema siku ya jumanne, atatoa ripoti kamili ya EU kuhusu mchakato mzima wa upigaji kura.
Amewataka washindani kukubali matokeo kwa sababu katika ushindani lazima mshindi apatikane ili aliongoze taifa katika kuleta maendeleo.
No comments :
Post a Comment