dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Tuesday, October 13, 2015

Vyama vyang'ang'ania mita 200 baada ya kupiga kura.

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec), Jaji mstaafu Damian Lubuva.
Baadhi ya vyama vya siasa nchini, vimesisitiza kwamba vitafuata Sheria ya Uchaguzi ya kukaa mita 200 kutoka vituo vya kupigia kura na siyo maagizo yanayotolewa na Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec), Jaji mstaafu Damian Lubuva, ya kuwataka wananchi kurudi nyumbani kusubiri matokeo baada ya kupiga kura Oktoba 25, mwaka huu.
 
Mara kadhaa Nec imekuwa ikivisisitiza vyama vya siasa kuwaelimisha wafuasi wao ili warudi nyumbani baada ya kupiga kura badala ya kukaa mita 200 kutoka vituoni kwa madai ya kulinda kura.
 
Katika maelezo yake, Nec imesema kwamba jukumu la kulinda kura litabaki kwa mawakala wa vyama na kwamba wananchi wanatakiwa kurudi nyumbani kusubiri matokeo. 
 
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Profesa Abdallah Safari, akizungumza na Nipashe jijini Dar es Salaam jana, alisema vyama vinafuata sheria na siyo maagizo ya Jaji Lubuva. Profesa Safari alisema sheria ipo wazi kwamba baada ya kupiga kura, mtu anatakiwa kukaa mita 200 kama anataka kusubiri matokeo ama anasubiri kitu kingine chochote na siyo kama anavyoagiza Jaji Lubuva.Alisema Nec haiaminiki kwa miaka mingi na kwamba inakuwa vigumu kwa vyama uchaguzi huu kuiamini na kuwashawishi wafuasi wao kurudi nyumbani kusubiri matokeo baada ya kupiga kura.
 
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa chama cha Alliance Democratic for Change (ADC), Said Miraaji, alisema Nec haiaminiki na kwamba itakuwa vigumu vyama kuwashawishi wafuasi wao kurudi nyumbani baada ya kupiga kura.
 
Alisema hoja ya Nec haijibiwi kirahisi badala yake lazima wadau mbalimbali washirikishwe kupitia vikao. Miraaji alisema Nec bado ina nafasi ya kujenga mazingira ya kuaminiwa na kwamba suala la wapigakura kukaa mita 200 kutoka vituo vya kupigia kura ni namna ya kuchukua tahadhari. 
 
Naye Katibu mkuu wa chama cha ACT-Wazalendo, Samson Mwigamba, alisema agizo la Nec la kuwataka wananchi kurudi nyumbani kusubiri matokeo halina maana na kwamba wao wanaangalia sheria inasemaje na siyo Jaji Lubuva anasema nini.
CHANZO: NIPASHE

No comments :

Post a Comment