Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Monday, October 26, 2015

Wanne mbaroni wakihusishwa jaribio la utekaji magari ya kura.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Ruvuma, Mihayo Msikhela
Watu wanne wanashikiliwa katika Kituo cha Polisi cha Wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma, wakidaiwa kutaka kuteka magari yaliyobeba vifaa vya kupigia kura.
Miongoni mwa vifaa hivyo ni masanduku yaliyokuwa na karatasi za kupigia kura na kwamba tukio hilo lilitokea eneo la Darpori wilayani Nyasa.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Ruvuma, Mihayo Msikhela, alisema jana kuwa maafisa wa serikali waliokuwa wakisafirisha vifaa hivyo walibaini kuwekewa vizingiti barabarani na waliposimama, watu hao walitoka porini na kuwazingira.
Kamanda Msikhela alisema ‘wavamizi’ hao walikuwa wameshika mapanga na silaha za jadi lakini walidhibitiwa na askari polisi waliokuwa kwenye msafara huo.
Katika tukio jingine, askari polisi katika manispaa ya Songea wametumia mabomu kuwatawanyisha watu walioandamana na kuifunga barabara ya kutokea mjini humo kwenda Mbinga.
Mtu mmoja ambaye jina lake halikupatikana mara moja anashikiliwa na polisi akihusishwa na kuwashambulia askari polisi waliokuwa wakidhibiti maandamano hayo. Kwa mujibu wa Msikhela, polisi inawatafuta watu wengine wanaodaiwa kuandamana isivyo halali na kusababisha vurugu kwa kuifunga barabara hiyo.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Ruvuma, Mihayo Msikhela, aliwaambia waandishi wa habari mjini hapa jana kuwa, tukio la kuandamana lilitokea juzi katika eneo la Lizaboni mjini humo. Msikhela alisema maandamano hayo yalifanyika baada ya kumalizika kwa mkutano wa mwisho wa kampeni za Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).
Alisema maandamo hayo yaliyomshirikisha pia mgombea ubunge wa Songea Mjini kupitia Chadema, Joseph Fuime, yalianzia eneo walilofanya mkutano na kwamba polisi ilipowataka watawanyike walikaidi.
“Baada ya wafuasi hao kutotii amri halali ya Jeshi la Polisi, tuliamua kutumia nguvu kutawanya maandamano hayo,” alisema.
Licha ya kuandamana, Msikhela alisema washiriki wa maandamano hayo waliwajeruhi askari polisi wanne kwenye sehemu mbalimbali za miili yao.
Alisema askari hao ambao hakuwataja majina walishambuliwa kwa mawe. Msekhela alisema polisi inaendelea kupeleleza  zaidi kuhusu tukio hilo la Fuime.
CHANZO: NIPASHE

No comments :

Post a Comment