dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Thursday, November 26, 2015

Kishindo cha Papa Francis Kenya

Rais Uhuru Kenyatta akijadiliana jambo na Papa Francis wakati alipowasili jana kwenye Uwanja wa Ndge wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta. Wengine kulia ni Makamu wa Rais, William Ruto na kushoto ni mke wa Rais Kenyatta, Margereth Kenyatta. Picha na AFP.
Nairobi, Kenya. Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Papa Francis aliyetua Nairobi jana saa 10:45 jioni, leo ‘atajichanganya’ katika moja ya majukumu muhimu wakati akiwa katika siku ya pili ya ziara yake nchini Kenya.
Jana, kiongozi huyo alipokelewa na mwenyeji wake, Rais Uhuru Kenyatta kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kinyatta (JKIA) na kisha wawili hao kufanya mazungumzo Ikulu kabla ya kukutana na maofisa wa Serikali na mabalozi.
Pia, kwenye uwanja huo wa JKIA, Papa Francis alipokewa na kwaya iliyokuwa ikiimba kwa kusema, ‘karibu Papa nchini Kenya’
Ratiba ya ziara ya kiongozi huyo inaonyesha kuwepo kwa mtiririko wa shughuli nyingi, kiwamo pia zile zenye sura ya kijamii.
Leo, anatarajiwa kukutana na viongozi wa dini mbalimbali na kisha kuongoza misa ya hadhara itakayofanyika Chuo Kikuu cha Nairobi.
Pia, amepanga kuwa na mkutano wa faragha na makasisi wa Kikatoliki kabla kutembelea makao makuu ya Mpango wa Mazingira wa Umoja wa Mataifa (UNEP).
Akiwa kwenye ofisi hizo zilizopo Gigiri, Papa Francis atatoa tamko maalumu kuhusu mazingira na mabadiliko ya tabianchi, hasa akiangazia mkutano wa kimataifa wa mabadiliko ya tabianchi utaofanyika baadaye mwaka huu nchini Ufaransa.
Ratiba hiyo inaonyesha kuwa kesho ikiwa ni siku ya tatu ya ziara yake nchini Kenya Papa Francis atazuru Mtaa wa Kangemi ambao una makazi duni na kukutana na watu zaidi ya 1,200.
Haikuweza kufahamika mambo atakayoyazungumza na watu hao, lakini habari zinasema kuwa huenda pia akagusia umuhimu wa kuwajali watu wenye kipato cha chini.
Kadhalika, Papa Francis atatembelea eneo la Uwanja wa Karasani na kuzungumza na makundi ya vijana na kukutana na maaskofu wa kanisa Katoliki katika uwanja huo wa michezo.
Papa Francis atawasili katika Uwanja wa Ndege wa JKIA nyakati za jioni, tayari kwa kuagwa na kuondoka kwenda Uganda kuendelea na ziara yake barani Afrika kwa ambayo itamfikisha Afrika ya Kati
Akiwa Uganda, Papa Francis anatarajiwa kukutana na mwenyeji wake, Rais Yoweri Museveni na baadaye wawili hao watakuwa na mazungumzo ya faragha na baadaye atapewa fursa ya kulihutubia taifa.
Jumamosi, akiwa bado nchini Uganda, Papa Francis anatarajiwa kuzuru eneo la kumbukumbu la Waanglikana katika eneo la Namugongo na kisha kuzuru eneo la mashahidi la Wakatoliki katika eneo lilo.
Pia, anatarajiwa kuongoza misa ya hadhara kwa ajili ya kumbukumbu ya Mashahidi wa Uganda na baada ya hapo atakutana na vijana wa Uganda kwenye Uwanja wa Ndege wa Kololo na baadaye kutembelea makao ya kutoa misaada kwa watoto.
Ratiba hiyo inaonyesha kuwa, Jumapili Papa Francis atakamilisha ziara yake nchini Uganda saa tatu asubuhi na kuelekea Jamhuri ya Afrika ya Kati, ambako atawasili Uwanja wa Kimataifa wa “M’Poko” mjini Bangui.
Baada ya kuwasili, Papa Francis anatarajiwa kuelekea moja kwa moja Ikulu ambako atakuwa na mazungumzo na mwenyeji wake na baadaye kukutana na mabalozi na viongozi wengine kabla ya kutoa hotuba.
Amepanga pia kutembelea kambi za wakimbizi. Baadaye atakuwa na mazungumzo na maaskofu wa Kanisa Katoliki na kisha kukutana na viongozi wa dini mbalimbali katika Chuo Kikuu cha Bangui. Papa Francis, pia anatarajiwa kuongoza misa ya hadhara katika Kanisa Kuu la Bangui na kutoa hotuba.
Nyakati za jioni, kiongozi huyo wa Kanisa Katoliki anatarajia kuongoza shughuli ya maungamo kwa vijana kabla ya kuongoza hafla ya maombi ya mkesha katika Kanisa Kuu la Bangui. Ataondoka baadaye kuelekea Rome, Italia akiwa amekamilisha ziara yake ya kihistoria barani Afrika.     

No comments :

Post a Comment