dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Sunday, November 29, 2015

Nipashe ilivyoibua kashfa ya makontena bandarini

  • Kama uhujumu uchumi kupitia utoroshwaji wa makontena ulioripotiwa na gazeti hili mwaka jana ungefanyiwa kazi, vigogo wa Mamlaka ya Mapato (TRA) na Mamlaka ya Bandari (TPA) wasingekumbwa na kadhia ya kusimamishwa kazi.

Lakini licha ya matoleo matatu kuchapisha uozo huo kutokana na uchunguzi uliofanyika kwa weledi, mamlaka husika zilipuuza na badala yake zikakanusha ikiwa ni pamoja na kupitia matangazo yaliyolipiwa kutokana na fedha za umma. 

Ingawa habari hizo hazikuzungumzia moja kwa moja makontena yote 349 yaliyotajwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, lakini mwelekeo wake ulilenga kuonyesha namna vitendo vya ukwepaji kodi kupitia utoroshwaji wa makontena, vilivyokithiri nchini hususan ni kwenye bandari hiyo.

Moja ya habari hizo ni ile ya Juni 22 mwaka jana, gazeti hili lilipoandika habari yenye kichwa Makontena yaondolewa kinyemela bandarini Dar.
Makontena yaliyobainika kwa wakati huo yalikuwa ni pamoja na yaliyotokea China na kuondolewa bandarini kinyemela.

Hatua hiyo ilifikiwa kwa maelezo kuwa makontena hayo yalikuwa ni mzigo wa kupita ukipelekwa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), lengo likiwa ni kukwepa kodi.

Makontena hayo yalibainika kubaki hapa nchini na kusambazwa kwenye soko.

Wahusika katika kadhia hiyo walifanikisha kuyatoa makontena hayo kwa kutumia vibali `feki’ na wakaguzi wakaruhusu magari ya kusafirishia mizigo kubeba makontena hayo licha ya kutokuwa na vigezo vya usafirishaji.

Nipashe ilijulishwa kuwa `mchezo mchafu huo na mingine ya aina hiyo imekuwa ikifanywa mara kwa mara na baadhi ya wafanyabiashara ili wasilipe kodi kwa kushirikiana na maafisa wa TRA wanaopokea rushwa nono.

Mamlaka za TRA na TPA zilipoulizwa kuhusiana na tukio hilo walianza kwa kueleza kwamba hawakuwa na taarifa kuhusiana na suala hilo.
TPA ilikanusha na kutolea ufafanuzi tukio hilo lakini kwa kukiri kuwapo kontena lililokamatwa huko Chang’ombe.

Taarifa ya TPA ilieleza kuwa  kulikuwa na jaribio la kutumia nyaraka za kughushi kuondoa kontena namba PCIU 298647-4 lililokuwa limepakiwa katika gari aina ya Scan namba T 425AAY/T318BXS.

Kwa mujibu wa TPA hatua hiyo ilifanyika kwa kutumia nyaraka za kughushi Juni Mosi mwaka jana.

TRA  ilipingana na taarifa ya TPA na kueleza kuwa (TRA) ilifuatilia kontena hizo na kulikamata moja huko Chang`ombe likiwa linapakua vitenge.

Nipashe ilizungumza na TRA kuhusiana na kutolewa kwa makontena kadhaa kwa njia za udanganyifu, Afisa mmoja alisema suala hilo linafanyiwa uchunguzi ili kubaini makontena mengine yaliyotoka kwa njia za udanganyifu, lakini hatima yake haijatangazwa hadi sasa.

Julai 27 mwaka jana, Nipashe liliendeleza habari ya uchunguzi yenye kichwa, TRA yahusishwa uondoaji mizigo kinyemela bandarini.’

Vyanzo vya gazeti hili bandarini hapo vilieleza maofisa wa TRA wasiokuwa waadilifu ni wahusika wakuu wa kutengeneza nyaraka za uongo kwa kushirikiana na wafanyabiashara ili kukwepa kodi.

Miongoni mwa mbinu zilizobainika kutumiwa na maofisa wa TRA ni kubadili kampuni za utoaji mizigo ili kuvuruga ushahidi ikiwa kampuni za awali ziliwekewa vikwazo.

Makontena yaliyohusishwa katika kashfa hiyo ni pamoja zilizozuiliwa mara kadhaa bandarini hapo ili kufanya uchunguzi kutokana na kasoro kadhaa zilizojitokeza.

Moja ya taarifa tulizochapisha ni kuhusu magari yanayotumika kubeba mzigo kwenda nje kulazimika kuwa na C65 na TI, miongoni mwa yaliyotumika kutorosha makontena kwa lengo la kukwepa kodi yakiwa na mihuri ya ‘seal’, hayakuwa na sifa na vigezo vya usafirishaji nje ya nchi.

Hata hivyo Nipashe ilipofuatilia suala hilo TRA, mamlaka hiyo haikutoa ushirikiano zaidi ya kujulishwa kuwa suala hilo limeshafanyiwa kazi.

Juzi, Rais John Magufuli alimsimamisha kazi Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Rished Bade na maafisa watano  kutokana na ubadhirifu wa makontena 349 kupitishwa kinyemela na kuisababishia serikali hasara ya Shilingi bilioni 80.
CHANZO: NIPASHE JUMAPILI

No comments :

Post a Comment