dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Sunday, November 29, 2015

TANI 332 WA CHAKULA NI MCHEZO MTUPU. NI SAWA NA TANI 100 ALIZOTOWA JK. WATU WATAKUFA NA NJAA VIJIJINI IRINGA!

Serikali yatoa tani 332 za chakula kijiji cha Mkukula




NA GEORGE TARIMO
29th November 2015.

Serikali imetoa tani 332 za chakula cha msaada kwa wanakijiji cha Mkulula wilayani Iringa wanaokabiliwa na upungufu wa chakula.

Aidha wananchi hao waliokuwa wakishindia ubuyu na matunda pori wamelalamika kuwa wanakula mlo mmoja kwa siku huku baadhi ya watoto wameshindwa kwenda shuleni.

Ukame uliotikisa baadhi ya vijiji vya wilaya hiyo umesababisha mazao kukauka, kwa mujibu wa maelezo ya wanakijiji waliyoyatoa kwa Mkuu wa Wilaya ya Iringa , Richard Kasesera.

Alifahamishwa hayo alipowatembelea na kuzungumza na wanakijiji cha Mkulula ambao ni waathirika wa njaa.

Japhet Mgimbuzi, akitoa kilio chake kwa Mkuu wa Wilaya alisema kutokana na hali mbaya ya hewa wanakula mlo mmoja lakini pia hawana fedha za kujikimu hali inayoongeza ugumu wa tatizo.

“Tunakula saa sita mchana hadi kesho tena hali hii inatuumiza tunaumwa vidonda vya tumbo kutokana na utumbo kukaa muda mrefu bila kula jamani, tunaomba serikali isikie kilio chetu. ”alisema Mgimbuzi
Kwenye mkutano wa hadhara viongozi wa Kijiji cha Mkulula na kata ya Malenga Makali walimwambia Mkuu wa Wilaya kuwa licha ya serikali kuwapatia msaada wa chakula mwezi Agosti, tatizo limeendelea kuwapo.

Kuna baadhi ya watoto hawaendi shule kwa kuwa hawajala chochote.
Baada ya kusikiliza malalamiko ya wananchi Kasesera aliahidi kutafuta chakula zaidi cha misaada.

“Nitaendelea kuomba chakula kutoka serikalini na hadi sasa chakula kimekuja kipo Makambako hela za kukisafirisha zimeshapatikana naishukuru Ofisi ya Waziri Mkuu.”

Aidha Kasesera aliwataka wakazi wa Iringa kuhifadhi chakula badala ya kuuza chote, huku akiwataka kujenga maghala ya pamoja ya kuhifadhi mahindi yatakayowasaidia wakati wa njaa.

Ofisa tarafa ya Isimani, Thomas Myinga, akizungumza kwenye ziara hiyo alisema changamoto kubwa inayowakabili wananchi na tarafa hiyo yenye kata sita ni upungufu wa mvua.

Mwenyekiti wa Kijiji cha Mkulula, Samweli Mbande alielezea zaidi kuhusu kukosekana kwa chakula hadi wanafunzi wanakwama kwenda shuleni.

Tuna changamoto ya ujenzi wa kituo cha afya lakini viongozi wanashindwa kukusanya michango kwa sababu kila wanapofika wanakuta hali ni mbaya, alisema.
CHANZO: NIPASHE JUMAPILI

No comments :

Post a Comment