dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Saturday, February 13, 2016

Bonge la mchepuko bandarini

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa (katikati) akiwa katika eneo lenye mabomba yanayotumika kupitisha mafuta kutoka kwenye meli kupitia Bandari ya Dar es slaam jana, wakati alipofanya ziara ya kukagua miundombinu yenye mianya ya ukwepaji kodi hasa kwenye mafuta yanayoingia nchini. Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu
By Florence Majani, Mwananchi 
Dar es Salaam. Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameendelea kuibua madudu zaidi ndani ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA) baada ya kugundulika kwa bomba la mchepuko lililokuwa likisambaza mafuta yanayokwepa kodi.
Akiwa katika ziara ya kushtukiza bandarini jana, Majaliwa alikagua namna mafuta yanavyopokelewa kutoka melini hadi yanaposambazwa kwa wafanyabiashara na kubaini kuwa kuna bomba lililochepuliwa kutoka bomba kuu ambalo huenda ndilo linalotumika kusambaza mafuta yanayokwepa kodi.
Kutokana na upotevu huo wa mafuta na kodi, Waziri Mkuu pia alimwagiza Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Aloyce Matei ahakikishe linajengwa bomba ambalo mamlaka hiyo itaweza kudhibiti moja kwa moja uingizwaji na usambazwaji wa mafuta kwa wafanyabiashara.
Waziri Majaliwa alitoa mwezi mmoja bomba hilo la mchepuko liondolewe na badala yake wote wanaotaka mafuta wachukue kutoka katika bomba moja tu ambalo TPA inaweza kulidhibiti.
Kadhalika Majaliwa alimwagiza Msajili Mkuu wa Hazina, Lawrence Mafuru kuvunja mkataba kati ya kampuni ya Tiper na Oryx na badala yake Tiper iendeshwe na Serikali kwa asilimia 100.
Kampuni ya Tiper inaendeshwa kwa ubia kati ya Serikali yenye asilimia 50 za hisa na Oryx Energies South Africa yenye asilimia 50.
“Kuanzia sasa nataka ufanye utaratibu wa kusitisha mkataba kati ya Oryx na Tiper na mambo mengine yatajulikana baadaye,” alisema.
Alisema lengo ni kuzuia upotevu wa kodi itokanayo na mafuta na kudhibiti wizi wowote wa mafuta bandarini.
Kadhalika katika ziara hiyo, Waziri Majaliwa alibaini kuwa Mamlaka ya Vipimo (WMA) waliufunga mtambo wa Tiper wa kutoa mafuta kwa madai kuwa unawapunja wafanyabiashara.
“Kwa nini WMA waufunge mtambo bila majadiliano na Serikali na wao wana uhakika gani kama wafanyabiashara wanapunjwa,” alisema.
Kutokana na kitendo cha WMA kufunga mtambo huo, Waziri Majaliwa alimwamuru mkurugenzi mtendaji wa wakala huyo, Magdalena Chuwa kuandika barua ya kujieleza sababu za kufanya hivyo.
“Nataka hadi saa 11:00 jioni awe ameandika barua ya kujieleza kwa nini afunge mita za mtambo huo unaoangalia namna mafuta yanavyotolewa. Inawezekanaje achukue maamuzi kama hayo ?” alihoji.
Kwa sasa Serikali imeanza ujenzi wa mtambo mkubwa wa mafuta ambao utakuwa ukipokea mafuta yote yanayotoka kwenye meli na kuyasambaza kwa wafanyabiashara.
Mtambo huo utakaoanza kazi Machi mwaka huu unatarajia kuondoa migogoro na changamoto za usambazaji wa mafuta, pamoja na kuratibu namna mafuta yanavyopokelewa na kusambazwa.
Hatua hiyo imekuja siku moja baada ya TPA kutangaza kuyafungia makampuni 210 yanayojihusisha na uagizaji mizigo kufanya kazi na mamlaka hiyo baada ya kubainika kwa kuipitisha bandari bila ya kulipia ushuru.
Katika kazi yake ya kwanza tangu aapishwe, Waziri Majaliwa alifanya ziara ya ghafla na kubaini makontena 349 yenye thamani ya zaidi ya Sh80 bilioni yaliyopotea bandarini hapo.
Siku chache baada ya kuteuliwa kuwa Waziri wa Uchukuzi, Makame Mbarawa alibaini upotevu wa makontena 11,019 na magari 2,019 kutoka bandari kavu (ICD), ambayo yaliisababishia Serikali kukosa Sh48.55 bilioni.    

No comments :

Post a Comment