dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Friday, February 5, 2016

Elimu bure yawachanganya watendaji Kata ya Kyanyari


By Florence Focus, Mwananchi 
Butiama. Waraka wa Serikali unaoelekeza elimu bila malipo, umesababisha mkanganyiko kwa viongozi wa Kata ya Kyanyari wilayani hapa Mkoa wa Mara baada ya kutakiwa kuchangia madawati.
Mkanganyiko huo ulitokea juzi kwenye kikao cha kuweka malengo na maazimio ya maendeleo ya kata hiyo.
Kaimu Ofisa Elimu Wilaya ambaye ni Ofisa Elimu Vifaa na Takwimu, Charles Michael aliwataka viongozi hao kuandaa mipango mikakati ya upatikanaji madawati kwa shule zote kwa kuwashirikisha wakuu wa shule.
Michael alisema mpango huo uwasilishwe ofisi ya mkuu wa wilaya haraka iwezekanavyo.
Alisema baada ya Rais John Magufuli kutangaza elimu bure, wazazi wamesitisha uchangiaji wa miundombinu ya elimu ikiwamo ujenzi wa vyoo vya shule, madarasa, nyumba za walimu na madawati.
“Wahimizeni wananchi wachangie miundombinu ya elimu, wakichangia hakuna makosa na kama mtasubiri Serikali elimu itakuwa bora elimu siyo elimu bora,” alisema Charles.
Diwani wa kata hiyo, Mgingi Muhochi alisema waraka uliotolewa na Serikali hauainishi iwapo wananchi wanapaswa kuchangia madawati, hivyo lazima ufafanuliwe upya.
“Siwezi kuwahimiza wananchi kuchangia madawati wakati waraka unajieleza, nitahitaji majibu na maelezo ya kutosha nitakapokuwa kwenye kikao cha baraza la madiwani ili wakati nawahamasisha kuchangia niwe na nyenzo ya kujitetea,” alisema Muhochi.
Mratibu Elimu Kata, George Bigori alisema kata hiyo ipo nyuma kwa elimu baada ya kuwapo kwa upungufu madarasa na walimu ikilinganishwa na idadi kubwa ya wanafunzi.
“Madarasa ni machache, wanafunzi wengi, walimu ni wachache ni vigumu kumkagua mwanafunzi ili kutambua kama ameelewa, darasa linajaa hadi sehemu ya kupita inakosekana, kiwango cha kufaulu lazima kishuke hata kama tutawafunga wanafunzi kengele ya usikivu,” alisema Bigori.     

No comments :

Post a Comment