dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Wednesday, February 3, 2016

Kigogo bomoabomoa arejeshwa kazini.

Baraza la Uhifadhi na Usimamizi wa Mazingira (Nemc).
Siku chache baada ya Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, kuwasimamisha kazi, vigogo watatu wa Baraza la Uhifadhi na Usimamizi wa Mazingira (Nemc), Kigogo aliyekuwa akisimamia bomoabomoa amerudishwa kazini, imebainika.
 
Kwa mujibu wa taarifa za ndani zilizolifikia Nipashe zinaeleza kuwa, kigogo aliyerudishwa kazini siku nne tu mara baada ya kusimashwa kazi ni Mwanasheria Mkuu wa Nemc, Heche Suguta.
 
Chanzo hicho kilieleza kuwa, Suguta alirudi kazini Januari 29, siku nne baada ya wizara hiyo kutangaza kumsimamisha kazi ili kupisha uchunguzi baada ya kutuhumiwa kukiuka miiko ya kazi katika kusimamia kiwanda cha Kusindika Minofu ya Punda kilichopo mkoani Dodoma.
 
“Heche yuko kazini tangu Ijumaa ya wiki iliyopita, alikaa nyumbani siku nne tu, ila hatufahamu nini kilitokea juu ya hilo,” kilibainisha. 
 
Chanzo hicho kilieleza kuwa, hawana taarifa za maofisa wengine kama watarudishwa kazini au laa.Mkurugenzi Mkuu wa Nemc, Bonventure Baya, alipoulizwa na Nipashe kuhusu suala la ofisa huyo kurudishwa kazini, alisema hawezi kuzungumzia jambo hilo kwa madai kuwa liko juu ya uwezo wake.
 
“Jambo hilo siwezi kulizungumza liko juu ya mabosi wangu, hivyo siwezi kusema chochote juu ya hilo,” alisema Baya.
 
Nipashe pia lilimtafuta Suguta ili kuzungumzia suala hilo, lakini simu yake iliita bila majibu na baadaye ilizimwa.
 
Maofisa wa wizara hiyo nao walitafutwa ili kuzungumzia jambo hilo, bila ya mafanikio, hadi Nipashe linakwenda mitamboni. 
 
Wengine waliokuwa wamesimamishwa kazi ili kupisha uchunguzi ni Ofisa Mazingira Mwandamizi, Dk. Eladius Makene na Ofisa Mazingira, Boniface Benedict Kyaruzi.
 
Katika adhabu hiyo, pia Baya, alitakiwa kuandikiwa barua ya onyo kali la mwisho kwa tuhuma ya udhaifu wa usimamizi wa watumishi wa Nemc, hivyo kusababisha malalamiko mengi kuhusu utendaji wa Baraza hilo.
 
Kuhusu kiwanda cha Kusindika Minofu, taarifa hiyo ilisema imegundulika kuwapo kwa ukiukwaji mkubwa wa makusudi na wa wazi wa miiko ya kazi kwa watumishi wa Nemc. 
 
Aidha, wizara iliagiza kuwa ndani ya wiki moja Nemc ipitie upya orodha ya wataalam na taasisi elekezi, zilizosajiliwa na kufuta wataalam na taasisi zote ambazo zimekuwa zikikiuka maadili ya kazi zao.
CHANZO: NIPASHE

No comments :

Post a Comment