dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Wednesday, February 10, 2016

UAE YAUNDA WIZARA MPYA ZA SERIKALI ‘FURAHA’ NA ‘UVUMILIVU’

Click here for the full cabinet



Waziri mkuu wa Miliki za Kiarabu UAE ametangaza kuundwa kwa wizara mpya ya furaha, uvumilivu pamoja na vijana huku akiahidi kuunda wizara nyingi zaidi.

Wizara hizo mpya imeundwa katika mabadiliko yaliyotekelezwa na utawala wa kiongozi wa UAE Sheikh Mohammed bin Rashid Al Maktoum.

Sheikh Maktoum, ambaye ni kiongozi wa Dubai amesema wizara mpya ya furaha inaazimia “kuchochea mtagusano baina ya wananchi wake mbali na kuhamasisha umma utosheke na kile walichonacho”.

Wizara mpya nyingine iliyoundwa ni “wizara ya kuvumiliana.”

Sheikh Maktoum vilevile ameagiza kuunganishwa kwa wizara nyingi mbali na kutoa zabuni za kuagiza makampuni kutoka nje kuendesha asilimia kubwa ya shughuli za serikali.

“Serikali sharti iweze kunyumbulika kwa urahisi. Nafikiiri hatuitaji wizara zaidi tunachoitaji ni mawaziri wenye uwezo wa kutafsiri mabadiliko na kuyatekeleza ipasavyo” Sheikh Makhtoum aliiambia kongamano la dunia linalojadili miundo ya utawala na serikali mjini Dubai.

“Tunachotaka ni serikali changa itakayokidhi matakwa ya vijana na umma.”

Wizara ya uvumilivu inanuiwa kupalilia nguzo muhimu ya jamii ya raia wa miliki za kiarabu ” alisema Sheikh Makhtoum kupitia mtandao wake wa Tweeter.

Vijana pia hawakusaulika aliunda baraza la vijana la taifa ‘Youth National Council’.

Wajibu wao mkubwa ni kuishauri serikali kuhusiana na maswala yanayowahusu vijana na wataongozwa na waziri mwanamke ambaye umri wake hautazidi miaka 22.

“Vijana ndio utawala ujao wa taifa hili” aliongozea Sheikh Makhtoum.


No comments :

Post a Comment