dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Tuesday, September 20, 2016

Tanzania imeonyesha utashi wa kisiasa kuwekeza katika Elimu - Ban Ki Moon!


Na  Mwandishi Maalum, New York

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon, amesema, utashi wa kisiasa, matumizi ya pato la taifa na matumizi ya fursa mbalimbali unaifanya Tanzania kuwa moja ya nchi ya mfano katika uboreshaji na upatikanaji wa elimu kwa wote.

Ban Ki Moon ameyatamka hayo siku ya jumapili, wakati wa hafla ya uzinduzi wa Ripoti ya Kamisheni ya Kimataifa kuhusu “ Kizazi kinachojifunza: Uwekezaji katika elimu kwa dunia inayobadilika”.

Hafla hiyo ilifanyika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa, na kuhudhuriwa karibu na Makamishna wote wanaounda tume hiyo akiwamo Rais Mstaafu wa Tanzania Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete.

Tume hiyo ambayo ipo chini ya uenyekiti wa Waziri Mkuu Mstaafu wa Uingereza ambaye pia ni Mjuumbe Maalum wa Katika Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Elimu, inawahusisha pia baadhi ya Marais waliopo madakarani, Mawaziri Wakuu waliopo madarakani na waliostaafu, Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Dunia, Mkurugenzi Mtendaji wa UNESCO, Wawekaziji wakubwa akiwamo Bw. Aliko Dangote, Taasisi za utafiti, wataalamu wa masuala ya fedha, asasi za kijamii na makundi ya vijana wakiwamo wanafunzi.“Uzoefu wa nchi kama Tanzania, Vietnam na nchi yangu mwenyewe Korea, unaonyesha kwamba pale ambapo pana utashi wa kisiasa, ukijumuishwa na uwepo wa fursa na raslimali fedha kuna kitu kinachowe kufanyika katika elimu.

Na kutokana na uzoefu wa nchi kama Tanzania na nyinginezo, Mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa amesema, Jumuiya ya Kimataifa ni lazima iwe tayari kuzisaidia kwa mitaji nchi ambazo zimeamua na kujituma katika kuifanyia mageuzi mifumo yake ya elimu na kujipati matokeo yanayoridhisha.

Jambo kubwa ambalo limetiliwa mkazo katika ripoti hiyo ni uwekezaji wa raslimali fedha. Kwanza, kwa kila nchi kukusanya kutumia mapato yake ya ndani, pili misaada kutoka mashirika ya kimataifa na taasisi za kimataifa, uwekezaji katika teknolijia ya mawaliano hususani internent ili kutoa fursa kwa wanafunzi kujipatia elimu na maarifa zaidi nje ya masomo ya darasani.

Akichangia majadiliano ya uzinduzi wa ripoti hiyo, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete kama mmoja wa Makamishna na ambaye pia aliongoza majadiliano kuhusu kipengele cha tatu cha mapendekezo ya ripoti hiyo kuhusu ujumuishi katika elimu. Kikwete alikuwa na haya ya kusema.

“Mafanikio ya elimu lazimia yamfikie kila mmoja wakiwamo wale wanaoishi katika mazingira magugumu na wanaobaguliwa wakiwamo wasichana”.

Akaongeza kuwa bahati mbaya leo hii Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara msichana mmoja kati ya ishirini wanaoishi katika maeneo ya umaskini ndiyo walio katika hatua za kumaliza elimu ya msingi.

Rais mstaafu Kikwete anaeleza kwamba takribani watoto milioni 75 ambao wamo katika umri wa kwenda shule wanakabiliwa kila siku na hatari moja ama nyingine. Idadi hiyo inajumuisha watoto milioni moja wa Syria ambao ni wakimbizi na ambao hawapati fursa ya kupata elimu.

“Kamisheni hii inaweka visheni ya kuwapatia fursa vizazi vijavyo huku mkazo ukitiliwa pia kwa wakimbizi,watoto wa mitaani,wasichana,watoto walioko katika ajira na makundi mengine ya jamii”. Akasema Rais mstaafu Kikwete.

Kiwango cha uwekezaji kinachotakiwa kuwekeza ni kiasi cha dola trillion 3 ifikapo mwaka 2030. Aidha kwa upande wa nchi ambazo uchumi wake ni mdogo zinatakiwa kuwekeza kutoka asilimia tatu ya pato lake hadi kufikia asilimia tano ya pato la taifa, wakati zile zenye uchumi wa kati zitatakiwa kuwekeza kutoka kiwango cha asilimia tano ya sasa hadi kufikia asilimia 5.7.

Ili malengo hayo ya uwekezaji yaweze kufikiwa, Makamishna kupitia ripoti yao wanatoa wito kwa Mawaziri wa Fedha kushirikiana na kufanya kati kwa karibu na Viongozi wao wakuu wa serikali.

Hata hivyo imeelezwa pia kupitia ripoti hiyo kwamba uwekezaji wa raslimali fedha si kigezo pekee cha kuwapatia fursa ya elimu kila mtoto mwenye umri wa kwenda shule.

Bali kinachotakiwa pia ni uwekezaji tangu mtoto anapokuwa tumboni kwa maana ya mzazi kupata lishe bora na huduma bora za afya, mtoto anapozaliwa kupata fursa ya lishe na makuzi bora, kuwa na fursa ya kupata elimu ya awali ambayo watafiti wanasema ni jambo la msingi sana katika kumuandaa mtoto.

Vile vile makamishna wamesisitiza haja na umuhimu wa walimu kuwa sehemu ya mabadiliko ya sekta ya elimu kwa wao wenyewe kupatiwa mafunzo ya mara kwa mara, kupewa motisha ya kutekeleza majukumu yao na kuachwa watekeleze kazi ya ufundishaji pasipo kuingiliwa au kuongezewa majukumu mengine ambayo yapo nje ya kazi yao ya ualimu.

Makamishna wanatahadharisha kupitia ripoti hiyo kwamba kama serikali hazitafanya haraka kuwekeza raslimali fesha katika elimu, watoto katika nchi zenye pato dogo la kiuchumi wataendelea kubaki katika dimbwi la umaskini huku wakiwa hawa ujuzi wala maarifa ya aina yoyote ile.

Ripoti inabainisha zaidi kwamba “ zaidi ya theruthi mbili ya watoto wenye umri wa kwenda shule katika nchi zenye kipato cha chini hawataweza kupata maarifa na elimu ya msingi ifikapo 2030 licha ya malengo ambayo jumuiya ya kiataifa imejiwekea ya kuhakikisha kila mtoto anakwenda shule”

Inaarifiwa kupitia ripoti hiyo kwamba ni nusu tu ya watoto wote wenye umri wa kwenda shule ya msingi na zaidi kidogo ya robo ya wanafunzi wa sekondari katika nchi zenye ukuaji mdogo wa uchumi au zile zenye uchumi wa kati ndio wanaopata fursa ya kujifunza maarifa/ ujuzi wa awali.

Vile vile ripoti hiyo imebaini pia kuwa watoto 330 milioni walioko katika shule za msingi na sekondari wanamaliza elimu yao wakiwa hawajaelimika.

Ripoti hiyo ni ukamilisho wa kazi ya mwaka mmoja ya uchambuzi uliohusisha zaidi ya taasisi 30 za utafiti, na mashauriano yaliyowahusisha zaidi ya washirika 300 kutoka nchi 105.

/ZanziNews.

No comments :

Post a Comment