dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Saturday, January 14, 2017

12 kuchunguza chanzo cha moto Uwanja wa JNIA!

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa akikagua eneo la mizigo lililoungua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) jana. (Picha na Mroki Mroki).

SIKU moja baada ya kutokea kwa moto katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano imeunda timu ya watu 12 kwa ajili ya kuchunguza chanzo cha moto huo.

Moto ulizuka juzi majira ya saa tano usiku katika chumba cha kuhifadhi mizigo kwenye jengo namba mbili (terminal II) na kuteketeza mizigo yote iliyokuwamo katika chumba hicho kidogo.

Tume hiyo imeundwa na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa ambaye alifika katika uwanja huo majira ya saa sita mchana akitokea mkoani Mwanza na kwenda moja kwa moja katika chumba hicho kilichoteketea ili kuona uharibifu uliojitokeza.

Akizungumza baada ya kutembelea eneo hilo, Mbarawa alisema, baada ya kutokea kwa moto huo hatua za haraka za kuuzima zilichukuliwa na kwamba wakati moto huo unatokea hakukuwa na mtu yeyote katika eneo hilo ambaye amedhurika.

Alisema baada ya kuzimwa kwa moto huo hatua ya pili ili kuwa ni kurejesha huduma ambapo walihamisha huduma kutoka katika jengo hilo kwenda katika jengo namba moja (terminal I) kwa kuwa kulikuwa na ndege ambazo zilikuwa uwanjani hapo.

“Tuliendelea kupeleka huduma zetu katika jengo la abiria namba moja na huduma ikaendelea kama kawaida, kwanza tulizima moto lakini pia tukawa tunaendelea na huduma kule. Huduma ziliendelea kule na wakati huo huo tukaja huku kutayarisha mifumo mingine kuhakikisha jengo hili liweze kutoa huduma muda mfupi baadaye,” alisema Profesa Mbarawa.

Alisema jambo la tatu ni kutafuta chanzo cha moto kwa kuwa moto hauwezi kutokea bila kuwa na sababu ya kitaalamu, hivyo timu hiyo itafanya kazi ya uchunguzi wa kina ili kubaini chanzo cha moto huo.

Alifafanua kuwa timu hiyo itafanya kazi kwa muda wa mwezi mmoja na itaoa majibu ya uhakika ya chanzo cha moto hiyo ambayo itasaidia kuweka mikakati ambayo itazuia matatizo ya moto katika viwanja vya ndege vyote nchini. “...ni timu ambayo ina watu wenye uwezo na ujuzi, ninaamini watatupa majibu ya uhakika, hawataupa majibu ya bahati mbaya ilitokea, kwenye utaalamu hakuna kitu bahati mbaya kuna sababu ya msingi, nategemea kupata ripoti ya kitaalamu inayosema chanzo ni nini,” alisema.

Alisema baada ya kupata ripoti hiyo wataweka mikakati ya kuzuia majanga ya moto katika viwanja vyote vya ndege nchini ili tukio hilo lisijirudie tena. Alisema kuwa kwa sasa hawawezi kumnyooshea mtu kidole, kwa kuwa kuna sababu ya kitaalamu.

Tume hiyo inaongozwa na Joseph Nyahende kutoka Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) imepewa kazi ya kutoa taarifa ya sababu za moto huo.

Hadi sasa thamani ya mizigo hiyo bado haijafahamika.

Moto huo ulizuka katika chumba kidogo kinachotumika kuhifadhia mizigo ya abiria wanaotoka nje ambayo huhifadhiwa hapo kutokana na mmiliki wake au mzigo huo kuchelewa kufika, inayohudumiwa na kampuni ya Swissport ambao ni wasimamizi wa mizigo yote inayopitia katika uwanja huo wa ndege.

No comments :

Post a Comment