Hili blog ni kuhusu Tanzania na dunia nzima kwa ujumla. Pita kila siku kwa habari moto moto. (This blog is about Tanzania and the world as a whole. Pass-by everyday for breaking news). ***********************KARIBUNI NYOTE / YOU ARE ALL WELCOME!***********************
Sunday, February 19, 2017
Sababu ya Burundi kukataa kushiriki mazungumzo ya amani mjini Arusha!
Serikali ya Burundi yagoma kushiriki katika mazungumzo ya amani ambayo yameandaliwa mjini Arusha nchini Tanzania ili kumaliza mzozo uliopo baina ya upinzani na serikali.
Wapinzani katika mmungano wa CNARED wamekubali kushiriki katka mkutano huo ambao umeanza Alhamis mjini Arusha.
Serikali kupitia msemaji wake Philippe Nzobonariba ameafahamisha kuwa serikali haijaridhishwa na uwepo wa wawakilishi wa kundi ambalo linahusika na jaribio la mapinduzi ya Mei mwaka 2015.
Kwa upande mwingine mshauri wa rais Pierre Nkurunziza amefahamisha kuwa muungano huo wa CNARED unajumuisha watu ambao wanatafutwa kujibu shtaka na vyombo vya sheria nchini Burundi na kusema kuwa muungano huo hautambuliki kisheria.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment