dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Saturday, March 18, 2017

Mfungwa aua mwenzake!

MWANAFUNZI wa Chuo cha Mafunzo ambaye amehukumiwa adhabu ya kifo, amemuua mfungwa mwezake wakiwa gerezani kwa kumpiga na kipande cha nondo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi, Hassan Nassir Ali, alisema tukio hilo lilitokea Jumatano wiki hii saa 8:00 mchana katika gereza la Kiinua Mguu, Kilimani, Mjini Unguja.

Alimtaja mfungwa aliyemuua mwezake kuwa ni Mawala Mdalasini Akilimani, ambaye ameshahukumiwa kunyongwa kwa kosa la mauaji lakini akiwa anasubiri adhabu hiyo ameua tena akiwa gerezani.

Alisema Akilimali alimuua Juma Rehani Hassan (56) ambaye pia alihukumiwa kunyongwa baada ya kutokea ugomvi baina yao na kupigwa hadi kufa.

Kamanda huyo alisema chanzo cha ugomvi wa wafungwa hao bado hakijajulikana na jeshi la polisi linaendelea na uchunguzi.

1 comment :

  1. Mawala Mdalasini Akilimani!!!!!
    Akilimali???? Wala sio uwongo. Akili kweli ni mali!!!

    ReplyDelete