dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Tuesday, March 28, 2017

Umuhimu wa mazoezi Ya Mwili Kwa Mgonjwa Wa Kisukari!


Kila mara tunashauriwa kuweza kufanya mazoezi kwa sababu mazoezi yana faida sana katika kuimarisha afya zetu, kuimarika kwa afya pekee yake haitoshi bali mazoezi ya mwili yanasaidia kwa kiwango kikubwa kuzuia magonjwa mengi sana.

Lakini kwa leo naomba tuangazie hasa umuhimu wa kufanya mazoezi kwa mtu mwenye kisukari, kwani kufanya mazoezi kwa mtu ambaye anaishi na ugonjwa wa kisukari kuna faida zifuatazo:

1. Mazoezi yanasaidia katika kudhibiti kiwango cha sukari katika mwili.

2. Yanasaidia kupunguza uzito wa mwili.

3. Mazoezi yanasaidia kudhibiti shinikizo la damu kwa kiwango kikubwa sana.

4 pia mazoezi yanasaidia kuweka kiwango cha mafuta kuweza kukaa katika hali nzuri.

5. Mazoezi ya mwili yanasaidia kupunguza msongo wa mawazo kwa kiwango cha hali ya juu sana, hii endapo utaamua kufanya kazi ushauri huu.

Baada ya kuona faida za kufanya mazoezi ya mwili, pia wataalamu mbalimbali wa afya, wanazidi kutuhimiza ya kwamba, mtu anatakiwa kutenga angalau nusu saa kwa ajili ya kufanya mazoezi kwa kila siku.

Hivyo zingatia yafuatayo  katika kufanya mazoezi:
Kama hujafanya mazoezi kwa muda mrefu, anza na mazoezi madogo madogo na kuongeza viwango taratibu vya baadhi ya mazoezi kila siku.

Pia mazoezi haya Unaweza kujiunga na gym, sehemu ambayo utapata mtaalamu wa kutoa mazoezi kwa watu wenye matatizo mbalimbali. Kupata mtu wa kukusaidia na kukuelekeza katika mazoezi kutakupa ari ya kufanya mazoezi kwa umakini zaidi. Isitoshe, gym zina vifaa vya kisasa vya kukupa vipimo vya mazoezi yako na maendeleo yako.

Kama huna uwezo wa kwenda gym wala usipate tabu, fanya mazoezi ambayo unayafahamu ambayo yatakufanya utoke jasho.  

/Muungwana.

No comments :

Post a Comment