dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Tuesday, May 16, 2017

PEMBA: MAMA ALIYEMUUWA MWANAWE NAYE AFARIKI!

Mwanamke aliekamatwa na polisi kwa tuhuma za kumua mtoto wake katika kijiji cha wingwi micheweni pemba nae amefariki dunia huku polisi na hospitali wakitupiana mpira kuhusu mazingira ya kifo chake.
Jeshi la polisi ambao walikuwa wakimshikilia mwanamke huyo wamesema alifariki akiwa hospiltalini lakini madaktari wamesema walipompokea mwanamke huyo kutoka kwa polisi akiwa tayari amefariki dunia.
Kamanda wa polisi mkoa wa kaskazini pemba Haji Khamisi Haji amesema waliamua kumpelaka hospitali mwanamke huyo baada kusema amebanwa na mafua ili ende kupatiwa matibabu.
Daktari aliyemfanyanyia uchunguzi marehemu huyo khalifan said salum amesema wamempokea mwanamke huyo kutoka kwa jeshi la polisi akiwa tayari ameshafariki dunia.
Amesema wakati anaendelea kumpima marehemu hyo walimkuta akiwa ametokwa na povu jingi mdomoni na hiyo kuchukuwa sampuli kwa ajili ya uchunguzi zaidi.
Hata hiyo mwandishi wa habari hizi akiwa anatoka katika hospitali ya michewi amemuona mtuhumiwa wa pili wa tukio hilo akiwa anapelekwa hospitali kwa kupatiwa matibabu akiwa na ulinzi kutoka jeshi la polisi.
/ Pemba News
Earlier report from Pemba:
http://zanzibarnikwetu.blogspot.ca/2017/05/baba-na-mama-watuhumiwa-kuua-mtoto-wao.html

No comments :

Post a Comment