airbnb

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Thursday, June 1, 2017

Historia ya Sheikh Abdulla Saleh Al-Farsy!

Image result for sheikh abdullah saleh farsy

Sheika Abdulla Saleh Farsy bila shaka alikua ni miongoni mwa wasomi wakubwa duniani, malenga na mwanahistoria . anakumbukwa kwa sura ya tabasamu na tabia njema alizokua nazo. Daima alikua na kundi la watu waliotaka kumsalimia au kuuliza maswali mbali mbali ya kidini. sifa zake zilifika hadi Somalia, Cape town na Malawi alikokua akifunza. Alihamia Kenya kutoka Zanzibar kwa kuhofia serekali ya wakati huo.

Sheikh Farsy alizaliwa Zanzibar tarehe 12, februari 1912 , kutoka familia yenye sifa ya elimu. Aliisoma Quran kutoka kwa Fatma Hamid Said (1854-1936) ambae ni mwanafunzi wa Sheikh
Amin bin Ahmed katika chuo cha kijiji cha jongeani ambako sheikh Abdulla alizaliwa na kulelewa.
Katika ulimwengu wa kiislamu wa waswahili alikua ni maarufu zaidi kuliko wengine. Mchango wake katika dini ya kiislamu ulikua ni wa kupigiwa mfano haswa baada ya kuandika tafsiri ya Quran iliyofahamika kama QURAN TAKATIFU ambayo ilikua ni tafsiri ya kwanza kabisa ya Kiswahili iliyo kubalika.Msomi huyu alikua na bahati sana kwa sababu wakati wake Zanzibar ilikua na vituo vya elimu ya kiislamu vilivyokua na vitabu na wasomi wa hali ya juu kam vile sheikh Abu Bakr bin Abdullah bin Bakathir (1881-1943)
ambae ni mwanafunzi wa Sayyid Ahmad bin AbuBakr Al-Sumait (1861-1925) sheikh huyu alikua ni msomi mkubwa alietambulika takriban kote Afrika mashariki na kati.Mwaka 1922 sheikh Farsy alijiunga na mskiti wa Barza baada ya kuamrishwa kufanya hivyo na walimu wake ambao ni Sayyid Hamid bin Mansab (1902- 1965) aliemfunza RISALATUL JAMIA, sheikh Hamid alikua ni imam katika mskiti wa Forodhani na alifariki akiwa anatowa darsa katika mskiti wa Gofu. Sheikh Hamid pia alikua ni mwanafunzi wa sheikh Muhammad Abdulrahman Makhzymy (1877-1946). Mwengine alikua ni sheikh Alwy bin Abdulwahhab ‏( 1902-1960 ) sheikh Alwy alimfunza sheikh Farsy vitabu 12 vya Fiqh , Lugh ya Kiarabu na kitabu
kilichofahamika kama MARDIFIN RABBIYYAH kuhusu mirathi.

Mbali na kuwa hodari katika fani za lugha ya kiarabu, aliandika mashairi kwa lugha ya kiarabu akiwa na miaka ishirini pekee hii ni kiuonyesha uwezo na elimu ya mashekhe wa Zanzibar wakati huo.

Sheikh Farsy pia hakuachwa nyuma katika elimu zenngine mbali na dini. Alikua mwanafunzi hodari katika masomo yake ya shule ya msingi na upili. Alijiunga na shule ya msingi mwaka 1924. Uerevu wake katika masomo ulimfanya mwalimu wake wa kiingereza ashindwe kujua kiwango chake. Mwanafunzi huyu alimaliza masomo yake ya shule ya msingi kwa mda wa miaka mitano badala ya minane.

Katika walimu wake mashuhuri wa shule alikua ni sheikh Abdullah bin Ahmad bin Seif (1900-1940) na sheikh Abdul Bary kutoka Al-Azhar University alieandikwa kazi kwa mda wa miaka ishirini na Sayyid Ali bin Humoud (1902-1911). Sheikh Abdul Bary alileta mchango mkubwa katika maendeleo zama za ukoloni kabla ya kuchapishwa kwa Quran Takatifu.

Tafsiri hiyo iliiga sana mfumo wa kitabu cha JALALAYN ambapo ilianza kuchapishwa mwaka 1956 na kufikia 1961 takriban juz 12 zilikua zimechapishwa. Kwa kukosa fedha kitabu hicho kilichelewa na kutoka mwaka 1969. Baada ya kudhaminiwa na Islamic Foundation. Sultan wa Qatar pia alitia mchango wake katika usambazaji wa tafsir hiyo kwa kutoa chapa 3,000.

katika miaka ya 1950 hadi 1960
kulikua na vuguvugu la Jamat-el-islamia lililopiga vita fikra na itikadi za Ahmadia, vuguvugu hili liliongozwa na sheikh Abdul Maudud (1903-1979) sheikh Farsy pia alikua ni mwanachama mkubwa wa vuguvugu hilo ila alikua na mfumo tofauti.

Baada ya kumaliza masomo yake katika chuo cha uwalimu (TTC) sheikh Farsy aliingia katika kazi ya ualimu wa shule ya msingi (1932-1947). Kupitia kazi zake za ubunifu na bidii alichaguliwa kama inspekta wa shule za msingi za Zanzibar na Pemba (1949-1952) Baadae alichaguliwa kama mwalimu mkuu wa shule ya upili ya kiislam (1952-1956). Aliondoka katika wizara ya elimu mwaka 1967 wakati alipokua mwalimu katika chuo cha uwalimu.

Mwaka 1960 alichaguliwa kama kadhi mkuu wa Zanzibar, ambapo alikua kadhi kwa mda wa miaka 7 hadi alipohamia Kenya baada ya vita vikali vilivyotokea Zanzibar na kusababisha vifo vya wengi, vita ambavyo vilieka historia na kuangaiwa Afrika nzima. Alikaribishwa Kenya na sheikh Muhammad Kassim Al-mazrui. Sheikh Farsy hakua maaruf Kenya kama alivyokua Zanzibar. sheikh Farsy alichaguliwa kama kadhi mkuu nchini Kenya na rais Jomo Kenyatta baada ya kupendekezwa na sheikh Muhammad Kassim Al-mazrui ambapo alikaa katika uongozi huo kwa mda wa miaka 14 hadi alipostaafu 1980.

Sheikh Abdulla Saleh Farsy aliiaga dunia Novemba 9, 1982, baada ya kuondoka Kenya kwa nda wa miezi minane alipokua ziarani Mascut, Oman. Kifo chake kiliwasikitisha wengi kwani alikua ni msomi alieacha athari kubwa na kumbukumbu Afrika mashariki.

No comments :

Post a Comment