WIZARA ya Elimu na Mafunzo ya Amali imeifunga skuli ya ‘Laureate International’ iliyopo Ole Kianga Wilaya ya Chake Chake Pemba, kutokana na tukio la kufariki kwa mwanafunzi Saleh Abdalla Massoud (11) wa darasa la nne mkaazi wa Limbali Wete, baada ya kupewa adhabu na mwalimu wa skuli hiyo.
Afisa Mdhamini Wizara ya Kazi, Uwezeshaji, Wazee, Vijana, Wanawake na Watoto Khadija Khamis Rajab ameeleza, kwa mujibu wa taarifa alizozipata kutoka kwa wanafamilia hao ni kwamba godoro la mtoto huyo lilichanika mfuko, ambapo alikwenda kuchukua solatep (gundi la karatasi) kugandisha ndipo mwalimu alieharibiwa kifaa chake kumpa adhabu ya kumtwisha godoro na kupitisha madarasa 13 huku akimpiga bakora, kusafisha vyoo vitano pamoja na koridoo, ambapo chooni alianguka na kuumia bega.
Waziri wa Kazi, Uwezeshaji, Wazee, Vijana, Wanawake na Watoto Mauldine Castiko amesema kuwa, kitendo alichokifanya mwalimu huyo, cha kumpiga na kumuumiza mwili marehemu ni udhalilishaji na kuvitaka vyombo husika kuchua hatua za kisheria dhidi yake.
Pemba News Media
No comments :
Post a Comment