dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Sunday, July 23, 2017

Japan: Roboti yagundua mafuta ya nuklia katika kinu cha Fukushima!

Roboti ya chini ya maji imenasa picha zinazoaminika kuwa za kwanza kabisa ya mafuta ya nuklia yaliyoyeyuka ndani ya kinu cha Japan kilichoharibiwa cha Fukushima.

Viwango vikubwa vya vitu vinayoonekana kama mawe vimeonekana katika kinu chake cha tatu.

Ikiwa itathibitisshwa itakuwa mafanikio makubwa kati oparesheni ya kusafisha kinu hicho.

Kinu hicho kulikumbwa na tsunamni mwaka 2011 na kusababisha ajali mbaya zaidi ya kinu cha nuklia tangu ile ya Chernobyl.Zaidi ya watu 200,000 walilazimika kuhama makwao kutokana na uchafuzi uliotoakana nakinu hicho.

Baadhi ya maeneo yaliyoharibiwa bado yana uchafu mbaya wa nuklia na toboti hutumiwa kuyasafisha.

Ugunduzi huo ulifuatia uchunguzi wa siku tatu wa kutumia roboti ndogo ya chini ya maji inayoitwa Little Sunfish.

Zaidi ya watu 18,500 waliuawa au kutoweka wakati tetemeko la ardhi lilisababisha tsunami kubwa ambayo ilisababisha ajali katika kinu cha Fukushina.

No comments :

Post a Comment