dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Sunday, August 20, 2017

Rais Shein ameelezwa Vijana 55 wamekubali kuachana na Dawa kulevya!

Zaidi ya vijana 50 wamekubali kuachana na utumiaji dawa za kulevya kufuatia ziara ya mkuu wa mkoa wa mjini magharibi katika maficho ya vijana hao huko kinazini ambapo mpaka sasa vijana hao wamepelekwa katika vituo vya kurekebisha tabia 'Sober House'.


Taarifa hiyo imetolewa na Ayoub mahmoud mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi mbele ya Rais ya wa Zanzibar na mwenyekiti wa baraza la mapinduzi Dkt Ali Mohamed Shein wakati akiwasilisha muhutasari wa utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika mkoa huo jana visiwani Zanzibar.
RC Ayoub amemueleza Rais Shein kuwa katika kuendeleza mapambano hayo mpaka sasa mashauri na kesi zimefikia 361 zinazowahusu watuhumiwa biashara za madawa ya kulevya na kwamba ziko katika hatua mbali mbali kwenye taratibu za kisheria.
Mkuu huyo wa mkoa yuko katika ziara ya siku tatu na Rais Shein ambayo imeanza jana katika Wilaya ya mjini na leo siku ya Ijumapili wataendelea na ziara katika wilaya ya Mjini magharibi 'A' na siku ya Ijumatatu atamalizia katika wilaya ya Magharibi 'B'


Ziara hiyo ni ya kwanza kwa Rais Shein tangu achaguliwe katika uchaguzi wa marudio mwaka jana, Na ni ya tatu tangu aingie madarakani mwaka 2010.

No comments :

Post a Comment