dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Tuesday, December 12, 2017

Umoja wa Ulaya watolea nje Netanyahu kuhusu Jerusalem!


Umoja wa Ulaya umetupilia mbali ombi la waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu kutaka Umoja huo utambue mji wa Jerusalem kama mji mkuu wa Israel.
Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa baada ya mkutano wa wawakilishi wa  mataifa ya Umoja wa Ulaya uliofanyika mjini Brussels Jumatatu, Umoja huo umetupilia mbali ombi hilo la waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu.

Benjamin Netanyahu aliitisha mkutano huo na Umoja wa Ulaya kutaka Umoja huo utambue Jerusalem kama mji wake mkuu.

Waziri mkuu wa Isarel alianza ziara yake nchini Ufaransa ambapo alifanya mazungumzo na rais Macron pia kuhusu suala hilo.

Federica Mogherini, kiongozi wa kidiplomiasia wa Umoja wa Ulaya amesema katika tangazo kuwa Umoja wa Ulaya unaunga mkono mikataba iliosainiwa kulinda mji wa Jerusalem.

Waziri wa mbmo ya nje wa Ujerumani Sigmar Gabriel hakushiriki katika kutano huo uliotolewa wito na waziri mkuu wa Israel.

No comments :

Post a Comment