dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Thursday, April 26, 2018

Kibano waagizaji bidhaa nje!

SERIKALI imezitaka kampuni zinazoagiza bidhaa nje kutekeleza matakwa ya sheria ya kulipa bima kwa bidhaa wanazoziagiza, vinginevyo watachukuliwa hatua kali.Hayo yalisemwa jana jijini Dar es Salaam na Kamishna wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (Tira), Baghayo Saqware, wakati wa mkutano wa nusu mwaka uliowakutanisha wadau wa bima kujadili mambo mbalimbali yanayohusu sekta hiyo.

Alisema watakuwa wanafuatilia kwenye Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ili kujua kama makapuni hayo yanalipa tozo ya bima kama sheria inavyowataka kwa kampuni zinazoagiza bidhaa nje.

Alisema wameangalia utekelezeaji wa sheria hasa kwenye mabadiliko ya sheria ambayo yalitaka waagizaji na waingizaji wa bidhaa kukatia bima bidhaa zao.

Saqware alisema sheria hiyo imeanza kutekelezwa mwaka huu na katika kipindi cha miezi mitatu wamepata tozo za bima Sh. milioni 409 ambazo zilikuwa zinakwenda nje.

“Wahakikishe wanapoagiza bidhaa nje ya nchi wanakata bima kutoka kwenye makampuni yaliyosajiliwa, lakini wanaweza kutumia mfumo wetu kukote walipo wakatumia bima za mizigo kutoka nje,” alisema.

Alisema utekelezaji wa suala hilo umekuwa na changamoto na endapo likitekelezwa itasaidia kuokoa fedha zinazopelekwa nje kwa ajili ya bima.

Aidha, alisema wamejadili matokeo ya utekelezaji wa maagizo na maelekezo ya serikali kuhusu sekta ya bima, “Tunaendelea kukusanya maoni kutoka kwa wadau wa bima ili kuboresha sekta ya bima nchini,” alisema.

Aidha, alisema sekta ya bima imekua kwa asilimia saba kama uchumi wa nchi unavyokua na matarajio yao baada ya mkutano huo wataweza kuongeza ukuaji wa sekta kwa kuangalia maeneo ambayo yanahitaji maboresho.

Pia, alisema changamoto kubwa ambayo inasababisha ukuaji wa bima nchini kuwa mdogo ni sera ya bima inahitaji kufanyiwa kazi na serikali, ufahamu wa wananchi kuhusu matumizi ya bima na kampuni kuongeza wigo katika bidhaa zao.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Kuendeleza Sekta ya Fedha Tanzania (FSDT), Sosthenes Kewe, alisema ukataji wa bima bado ni changamoto kwa wananchi, jambo ambalo linatakiwa kufanyiwa kazi .

Alisema kuna kazi kubwa ya kuwaelimisha wananchi ili wajue umuhimu wa kukata bima ili ziwasaidie wanapopatwa na majanga.

No comments :

Post a Comment