dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Monday, August 20, 2018

Polisi wapambana na waandamanaji wanaomuunga mkono Bob Wine!


Vikosi vya usalama nchini Uganda vimetumwa kuzima maandamano kwenye mji mkuu Kampala kupinga kukamatwa kwa Robert Kyagulanyi mwanasiasa wa upinzani ambaye pia anafahamika kama Boni Wine.

Waandamanaji wanachoma moto magurudumu ya magari, wanarusha mawe huku pia wakiweka vizuizi vya barabarani.

Wengi wanayaona mashataka hayo kama yaliyochochewa kisiasa.Wanajeshi na polisi wanaweza kuonekana wakiwa juu ya magari wakipita kati kati mwa mji. Sehemu zingine za mji wa kampala maafisa wa usalama wamefyatua risasi hewania na kurusha vituo machozi kutawanya waandamanaji.

Misukosuko inaongezeka mjini Kampala kufuatia kukamatwa kwa mbunge Bobi Wine. Ripoti zimeibuka kuwa aliteswa akiwa mikononi mwa wanajeshi. Rais Yoweri Museveni amekana madai kuwa Bobi Wine alijeruhiwa.

Watu kadhaa wamekamatwa akiwemo mwandishi wa habari wa Reuters aliyekuwa akifuatilia ghasia hizo.

Wiki iliyopita Bobi Wine 32, na watu wengine walishtakiwa baada ya kampeni za kuelekea uchaguzi mdogo eneo la Arua kaskazini mwa nchi. Polisi wanasema walikuwa wamewaongoza wafuasi wao kushambulia msafara wa Rais Museveni.

No comments :

Post a Comment