dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Saturday, September 22, 2018

Kangi Lugola amuagiza IGP kuwakamata watu hawa kuhusu ajali ya Mv Nyerere!

Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola amuagiza IGP Simon Sirro kuwakamata na kuwachukulia hatua wote wanaotumia ajali ya kivuko cha Mv Nyerere iliyotekea Alhamisi kama mtaji wa kisiasa.

Waziri Lugola ametoa agizo hilo leo Septemba 22 alipowasili katika eneo la tukio kilipozama kivuko hicho huko Ukara,Ukerewe mkoani Mwanza, akitokea mkoani Kigoma ambapo amesitisha ziara yake ya kikazi na kuelekea Jijini Mwanza kufuatilia ajali hiyo.Akizungumza katika eneo la tukio Waziri Kangi amesema, serikali inaendelea na zoezi la uokoaji na uopoaji hadi hatua ya kivuko kuondolewa majini, wakiamini bado kuna watu walio hai, huku akiwaonya Wanasiasa na watu wanaochukua tukio hilo na kulifanya kama mtaji wa kisiasa kuacha kufanya hivyo badala yake watumie nafasi hii kuwaunganisha Watanzania.

''Wale walioanza kutoa taarifa zao za kitakwimu juu ya kinachoendelea hapa tutatumia sheria ya takwimu kuwakamata na kuwashtaki pia wanaoendelea kusambaza kwenye mitandao taarifa zisizo na ukweli IGP, nakuagiza kupitia vitengo vyetu vya makosa ya kimtandao kuwakamata ili tuwashtaki" amesema Waziri Lugola.

No comments :

Post a Comment