WAKATI wimbi la viongozi,wabunge na madiwani wa vyama vya upinzani kuhamia Chama Cha Mapinduzi likishika kasi, Mbunge wa Kilwa kusini, Seleman Bungara (Bwege) amesema hawaendi CCM kwasababu ya kuvutiwa na utendaji wa serikali ya awamu ya tano. Bali wananunuliwa na kutishwa.
Bwege ameyasama hayo leo katika kijiji cha Kiranjeranje wakati wa mkutano wa hadhara baada ya kupewa nafasi awasalimie wananchi waliokuwepo kwenye mkutano huo ambao msemaji wake alikuwa mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Kilwa, Abou Mussa.Bwege licha ya kusema baadhi ya madiwani wanaotokana na chama hicho wilayani humu kuombwa wahamie CCM kwa ahadi ya kupewa fedha lakini hata yeye ameendewa mara nyingi na kushawishiwa ahamie katika chama hicho tawala.
Alisema baadhi ya madiwani wanaotokana na chama hicho waliombwa wahamie CCM kwa ahadi ya kupewa fedha na kurejeshwa kwenye nafasi zao kupitia chaguzi kwa madai kwamba wanahakikishiwa watashinda kwa njia zozote.
"Tumefika mahali diwani anaambiwa aache udiwani apewe udiwani na mbunge aache ubunge ili apewe ubunge tena.Wengine wanatishwa baada ya kukataa, Kwa sasa hakuna demokrasia,"alisema Bwege.
Aliwambia wananchi hao kwamba mpango wa CCM ulikuwa ndani ya miaka miwili wawachukue madiwani tisa ili halmashauri ya wilaya hii iongozwe na CCM kwa mara nyingine.Hata hivyo mpango huo umeshindwa kufanikiwa.Badala yake wamehama madiwani watatu tu.

No comments :
Post a Comment