Maziko ya Mtangazaji wa RTD Ahmed Jongo yamefanyika leo makaburi ya Mbagala Charambee Dar es Salaam.
Mtangazaji mkongwe na mmiliki wa redio ya Sports FM Abdallah Idrisa Majura akijumuika na ndugu, Jamaa na marafiki kupata chakula nyumbani kwa marehemu Tandika Maghorofani leo mchana kwenye mazishi ya aliyekuwa Mtangazaji mkongwe wa Radio Tanzania (RTD),Ahmed Jongo.
Sehemu ya waombolezaji wakiwamo ndugu, jamaa na marafiki wakijadiliana jambo nyumbani kwa marehemu aliyekuwa mtangazaji nguli wa Radio Tanzania (RTD),Ahmed Jongo, nyumbani kwake Tandika Maghorofani,jijini Dar es Salaam, wakiwemo wacheza kandanda nyota wa zamani akiwemo (kutoka kulia) Suleiman Mkati, Kaburu, Mohamed Hussein Mmachinga pamoja na mafundi mitambo wa toka enzi za RTD Mzee Ali Saidi Tunku na Juma Kengele.
Miongoni mwa ndugu, jamaa na marafiki wakiwa katika picha ya pamoja wakiwa nyumbani kwa aliyekuwa Mtangazaji mkongwe wa Radio Tanzania (RTD),Ahmed Jongo Tandika Maghorofani ambaye amefarikia dunia jana. Kutoka kulia ni mwanamuziki mkongwe Waziri Ally wa Njenje (zamani Msondo Ngoma) fundi mitambo James Mhillu, Adam Gille na Ankal.
Watangazaji, mafundi mitambo wacheza kandanda nyoya wa enzi hizo na viongozi wa soka wakipata picha ya kumbukumbu baada ya kujumuika na ndugu, jamaa na marafiki nyumbani kwa marehemu aliyekuwa Mtangazaji mkongwe wa Radio Tanzania (RTD),Ahmed Jongo Tandika Maghorofani,jijini Dar es Salaam.
No comments :
Post a Comment