dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Tuesday, June 18, 2019

Aliyekuwa Rais wa Misri, Mohammed Morsi azikwa alfajiri ya leo!

Mwili wa aliyekuwa Rais wa Misri, Mohammed Morsi umekwisha zikwa mapema alfajiri leo ikiwa ni saa chache tangu afariki dunia akiwa katika viunga vya Mahakama.

Mwanasheria wake ameliambia Shirika la Habari la AFP kwamba Morsi, amezikwa Mashariki mwa jiji la Cairo mapema huku familia yake ikishuhudia.

Mtoto wake, Abdullah Mohammed Morsi, amebainisha kwamba serikali iliwakatalia ombi lao la kufanya mazishi ya umma katika moja ya kijiji alichokulia Baba yake.
Mashirika ya haki za binadamu na wanaharakati wamekua wakipigia kelele suala la afya yake na namna serikali ilivyomtenga kuchangamana na watu. Morsi,67 alikua gerezani tangu alipopinduliwa na jeshi mwaka 2013.

No comments :

Post a Comment