airbnb

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Friday, August 30, 2019

MAANDAMANO UBALOZI WA AFRIKA YA KUSINI KATIKA SURA YA KIDIPLOMASIA!

Jumatano ya tarehe 28/8/2019 jjji la Dar es Salaam limeshuhudia baadhi ya vijana wakiandamana katika Ubalozi wa Afrika ya Kusini nchini Tanzania wakitaka kuachiwa kwa ndege ya Tanzania inayoshikiliwa kwa amri ya Mahakama ya Gauteng nchini Afrika ya Kusini.

Awali Serikali kupitia Msemaji wa Serikali Dr. Hassan Abbas ilitoa tamko juu ya hatua zilizokwisha chukuliwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania zikiwemo za Kisheria na za Kidiplomasia katika kuhakikisha Tanzania inapata haki yake kufuatia kukamatwa kwa ndege hiyo.

Serikali kwa kutambua kuwa suala hilo ni la kisheria kwa maana lipo mahakamani, imeacha Mahakama zifanye kazi yake.
Ingekuwa vema zaidi kwa watu walioandamana kufahamu hili kwanza kabla ya kutumia utaratibu waliotumia.

Mbali na hilo kwa mujibu wa maelezo ya Kamanda wa Kanda Maalumu Dar es Salaam DCP Lazaro Mambo sasa ni kwamba waandamanaji hawakuwa na kibali cha Polisi hivyo kuyafanya maandamano yao kuwa batili.

KIDIPLOMASIA UBALOZI UNAWEZA KUINGILIWA?

Kwa mujibu wa Mkataba wa Vienna wa Mwaka 1961 unaohusu Mahusiano ya Kidiplomasia yaani Vienna Convention on Diplomatic Relations of 1961 unaeleza kama ifuatavyo katika Ibara ya 22 (1 na 2) ninanukuu:

Article 22

1. The premises of the mission shall be inviolable. The agents of the receiving State may not enter them, except with the consent of the head of the mission.

2.The receiving State is under a special duty to take all appropriate steps to protect the premises of the mission against any intrusion or damage and to prevent any disturbance of the peace of the mission or impairment of its dignity.

Kwa tafsiri yangu:

"Maeneo ya Ubalozi hayaruhusiwi kuingiliwa na Nchi iliyompokea Balozi isipokuwa kwa kibali cha Balozi husika wa nchi hiyo"

*Pili, nchi iliyompokea Balozi ina wajibu wa kuulinda ubalozi dhidi ya uingiliwaji wowote wa maeneo ya ubalozi ama uharibifu ama kuvunjwa kwa amani yoyote ya Ubalozi."*

Hii ndiyo sababu wale walioandamana walikamatwa na Polisi kwa sababu Mkataba unaitaka nchi iliyompokea Balozi iulinde ubalozi dhidi ya athari zinazoweza kuupata ubalozi kama ilivyoelezwa kwenye Mkataba.

Hivyo basi kulikuwa na umuhimu kwa waandamani kutambua haya kabla ya kuandamana.

Ni imani yangu na kama alivyosema Msemaji Mkuu wa Serikali Dr Hassan Abbas kuwa suala la ndege litatuliwa kisheria na Kidiplomasia hivyo sisi Watanzania tuwe na subira na imani juu ya Serikali katika utendaji wake.

Kuandamana kunaweza kukawa ni kuonesha hisia za watanzania katika kuunga mkono juhudi za Rais Dr. John Pombe Joseph Magufuli lakini ilikuwa muhimu zaidi kufahamu Mkataba wa Vienna ili kutoleta mgogoro wa Kidiplomasia baina ya Tanzania na Afrika ya Kusini kwa kuwa nchi hizi mbili zina historia ya pekee ya undugu ambayo si vema sisi watanzania tukaichafua.

Asanteni.

Ndimi:

Abbas Mwalimu (Facebook & Instagram)

+255 719 258 484.

No comments :

Post a Comment